Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 14.02.2022: Kounde, Rice, Tielemans, Broja, Leao, Sterling, Araujo - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Sunday, 13 February 2022

Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 14.02.2022: Kounde, Rice, Tielemans, Broja, Leao, Sterling, Araujo

 

Jules Kounde

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Chelsea imeuweka usajili wa mlinzi wa Sevilla na Ufaransa Jules Kounde, 23, kama kipaumbele chake cha kwanza wakati wa usajili wa majira ya joto huku "The Blues" hao wakimtaka pia kiungo wa West Ham na England Declan Rice, 23, pamoja na kiungo wa Monaco mfaransa mwenye umri wa miaka 22 Aurelien Tchouameni. (Telegraph - subscription required)

Meneja wa Leicester Brendan Rodgers anasema timu hiyo inapaswa kuwa wa kweli kuhusu hatma ya kiungo wake wa kimataifa wa Ubelgiji Youri Tielemans, 24, ambaye anaingia katika miezi 18 ya mwisho ya mkataba wake akihusishwa na klabu za Arsenal na Manchester United. (Metro)

Arsenal inafikiria kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Armando Broja, 20 wakati wa majira ya joto. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Albania kwa sasa anafanya vyema akiwa kwa mkopo na klabu ya Southampton. (Football London)

Armando Broja

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Juventus wako tayari kusikiliza ofa kwa ajili ya kiungo mfaransa Adrien Rabiot, 26, na mlinzi wa kushoto Mbrazil Alex Sandro, 31. (Gazzetta dello Sport, in Italian - subscription required)

Barcelona inatarajia kuzima nia za vilabu vinavyomtaka kiungo wake Mhispania Gavi, 17, na beki wa Uruguay Ronald Araujo kwa kuwapa mikataba mipya wachezaji hao. Liverpool na Manchester United zinamuania Araujo mwenye miaka 22. (ESPN)

Mshambuliaji wa AC Milan na Ureno Rafael Leao, 22, anasakwa na vilabu vya Arsenal na Newcastle katika dirisha lijalo la usajili. (Fichajes, in Spanish)

Rafael Leao

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Mauricio Pochettino anafikiria kuikacha Paris St-Germain msimu huu baada ya kutofautiana na baadhi ya maafisa waandamizi wa klabu hiyo. (Goal, in French)

Manchester United inamuwania mlinzi wa Borussia Monchengladbach Ramy Bensebaini, 26, ikimtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Algeria kuziba nafasi ya mlinzi wa kushoto wa England Luke Shaw. (Fichajes, in Spanish)

Pep Guardiola anataka Raheem Sterling, 27, asaini mkataba mpya kusalia Manchester City lakini anasema klabu hiyo itakua na uamuzi wa mwisho kuhusu hatma ya mshambuliaji huyo wa England.

Raheem Sterling

CHANZO CHA PICHA,REX FEATURES

Mkataba wa sasa wa Sterling unamalizika June 2023 akikiri kuwa milango iko wazi kukipiga nje ya England. (Guardian)

West Ham na Atalanta zilikubalina kuhusu uhamisho wa mshambuliaji raia wa Colombian Duvan Zapata, 30, kabla ya mpango huo kukwama masaa machache kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.

Kwa sasa West ham inayonolewa na David Moyes imesalia na mshambuliaji mmoja wa maana Michail Antonio. (ESPN via Football Italia)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here