Arsenal bado wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Uhispania Alvaro Morata, 29, ambaye yuko kwa mkopo Juventus kutoka Atletico Madrid . (Clciomercato, via The Boot Room)
Kocha wa Manchester City Pep Guardiola anataka klabu hiyo kuongeza mkataba wa mshambuliaji wa Uingereza Raheem Sterling, 27. (Fabrizio Romano on Twitter).
Houston Dynamo wametoa ofa ya kumsajili kiungo wa kati wa Atletico Madrid na Mexico Hector Herrera, 31. (MLS)
Mlinzi wa Real Madrid Lucas Vazquez, 30, anataka kuondoka katika klabu hiyo ili kucheza soka katika kikosi cha kwanza ili aweze kuwa katika kikosi cha Uhispania kwenye Kombe la Dunia. (El Nacional, in Spanish)
Vilabu vitatu vya Italia Inter Milan, AC Milan na Juventus wote wanavutiwa na mshambuliaji wa Barcelona na Uholanzi Memphis Depay, 28. (Sport, in Spanish)
Tottenham wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili mlinzi wa Inter Milan na Uholanzi Stefan de Vrij, 30. (InterLive, via Star).
Everton inaweza kujaribu kumsajili mmoja wa wachezaji watatu wa Chelsea wanaocheza kwa mkopo Billy Gilmour, Conor Gallagher au Armando Broja msimu huu wa joto. Kiungo wa kati wa Scotland Gilmour, 20, yuko Norwich, kiungo wa kati wa Uingereza Gallagher, 22, yuko Crystal Palace naye mshambuliaji wa Albania Broja, 20, yuko Southampton. (Givemesport)




No comments:
Post a Comment