Urusi na Ukraine: Ni zipi hatari za shambulio la kinyuklia? - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Monday, 28 February 2022

Urusi na Ukraine: Ni zipi hatari za shambulio la kinyuklia?

 

Russia's Poseidon nuclear-armed underwater vehicle

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Video ya gari la mtambo wa nyuklia wa Urusi ulio chini ya maji wenye silaha za nyuklia lenye uweze wa kujiendesha kufanya mashambulio unaofahamika kama Poseidon nuclear -armed underwater vehicle - ilichukuliwa na Tass, Shirika la habari la taifa la Urusi.

Jumapili, Rais Putin aliagiza jeshi lake kuhamisha " vikosi vya kudhibiti" - ambavyo vinajumuisha silaha za nyuklia ''kufanya jukumu la mapambano maalumu''. Lakini hilo linamaaninisha nini hasa?

Haiko wazi kabisa, wanasema wachambuzi wa Magharibi wanasema,. Maafisa wa uingereza wanasema kwamba lugha iliyotumiwa na Putin haiendani na uelewa wao wa viwango vya tahadhari kwa silaha za nyuklia za Urusi.

Baadhi wachambuzi wanafikiria Puti alikuwa anaamrisha hatua ya chini abisa ya tahadhari , "mara kwa mara", kuelekea hatua inayofuata ya juu , "ya juu zaidi", (yenye ''hatari ya kijeshi'' na "kamili " bado ni ya juu) lakini hilo lilikuwa isio ya kuaminika . Kila hatua inaongeza utayari kwa ajili ya matumizi ya silaha.

Wengi hatahivyo wamefasili hatua hiyo kimsingi kama aina ya kutoa kiashiria kwa umma, kuliko kuonyesha lengo halisi la kutumia aina hizo za silaha, ambazo Putin anafahamu kuwa zitaleta ulipizaji kisasi wa Magharibi. Waziri wa ulinzi wa Uingereza Ben Wallace amedokeza kuwa anaamini kuwa kimsingi tangazo la Putin lilikuwa ni kwa lengo la ''kuvutia ushawishHilo halimaanishi kwamba hakuna hatari na huenda hali ikahitaji kufuatiliwa kwa karibu.

Je lilikuwa ni onyo la kwanza?

Wiki iliyopita, Putin alionya kwa lugha ya mafumbo zaidi kwamba kama nchi nyingine zitaingilia mipango ya Urusi zitakabuiliwa na athari "jambo ambalo halijaonekana kabisa ". Hilo lilitafsiriwa kama onyo kwa Nato la kutohusika moja kwa moja kijeshi katika nchini Ukraine.

Nato kila mara imekuwa wazi haitafanya hilo, ikifahamu kuwa inaweza kusababisha mzozo wa moja kwa moja na Urusi ambao unaweza kuchochea vita vya nyuklia. Onyo la Jumapili lilikuwa la moja kwa moja zaidi na la umma.

Putin alisema hatua hiyo ilikuwa ni kujibu "kauli za uchokozi". Jumatatu, Kremlin alisema hii ilimaanisha kauli zilizotolewa na maafisa wa Magharibi ,ikiwa ni pamoja na kauli iliyotolewa na Waziri wa mambo ya nje wa Liz Truss, kuhusu uwezekano wa migongano na makabiliano na Nato.

Maafisa wa magharibi pia wanaamini kuwa onyo jipya limekuja kwasababu Putin hakuelewa uwezo wa kijeshi wa Ukraine.

Huenda alidhani kiwango cha upinzani wa kijeshi atakaokabiliana nao kutoka Ukraine ni wa kiwango cha chini. Na alifikiri kiwango cha kuungana kwa mataifa cha magharibi katika kuweka vikwazo vigumu ni cha chini. Hilo lilimfanya hana la kufanya ila kuongea kwa ukali na kuchukua hatua mpya.

"Hii ni dalili ya hasira, kukanganyikiwa na kukata tamaa," Jenerali wa Ulingereza aliyestaafu hivi karibuni alisema.

Balozi wa Marekani katika Umoja wa mataifa Linda Thomas-Greenfield alisema lugha hii ni sehemu ya juhudi za Putin za kuhalalisha vita katika Ukraine kwa kudai sio ya mchokozi bali inakabiliwa na tisho na kwa hiyo inataka kujiinda.

Ikiangaliwa hivi, tahadhari ya nyuklia ni njia ya kusisitiza ujumbe huu kwa watu. Njia nyingine ya kuliangalia hili ni kwamba Putin ana wasi wasi juu ya mipango ya Magharibi ya kutoa usaidizi wa kijeshi kwa Waukraine na anataka kuwaonya juu ya kutofanya hilo sana.

Sababu nyingine ni kwamba anaogopa vikwazo, ambavyo alivielea katika tangazo lake, kama vilivyobuniwa kwa ajili ya kusababisha mzozo na kupindua serikali yake. Lakini kwa ujumla ujumbe unaonekana kuwa ni onyo kwa Nato kwamba kama itahusika moja kwa moja matukio yanaweza kuwa mabaya.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here