DR Congo: FARDC yaishtumu Rwanda kwa kuisaidia M23 - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Tuesday, 29 March 2022

DR Congo: FARDC yaishtumu Rwanda kwa kuisaidia M23

 

Sultani Makenga (file photo)

CHANZO CHA PICHA,AFP

Maelezo ya picha,

Sultani Makenga, mpiganaji mkuu, anaaminika kuwa miongoni mwa viongozi wa M23

Jeshi la DR Congo (FARDC) limesema kuwa wapiganaji wa M23 wakisaidiwa na jeshi la Rwanda walishambulia milima ya Chanzu na Runyoni huko Rutshuru.

Msemaji wa Jeshi la Rwanda (RDF) aliambia BBC kwamba "jeshi la Magharibi halikuwa vitani kote DRC".

Mjini Goma Jumatatu jioni, Brig Jenerali Sylvain Ekenge, msemaji wa serikali ya Kivu Kaskazini, aliwaambia waandishi wa habari kwamba wanaume wawili waliovalia mavazi ya kiraia wametambuliwa kuwa wanajeshi wa Rwanda waliokamatwa na wapiganaji wa M23.

Taarifa kutoka upande wa Rwanda ilisema watu hao "walikamatwa mwezi uliopita" na kwamba majina yao yalisambazwa kwa idara ya upelelezi ya Kongo katika mkutano wa pamoja wa pande hizo mbili Februari 25 (2) mjini Kigali.

Rwanda yakanusha kuhusika na mashambulizi ya DR Congo

Gavana wa jimbo la magharibi mwa Rwanda amekanusha madai ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwamba Kigali inaunga mkono waasi wa M23.

Francois Habitegeko katika taarifa yake alitaja madai hayo kuwa yasiyo na msingi na uongo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here