Je, mlo wa majimaji ni salama katika kupunguza uzito haraka? - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Sunday 13 March 2022

Je, mlo wa majimaji ni salama katika kupunguza uzito haraka?

 

Blending vegetables into a juice

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Lishe inayotegemea juisi ya matunda na mboga mboga huwa na kiwango cha juu cha vitamini lakini kalori, proteni na ufumwele huwa kidogo

Shane Warne, ambaye alifariki dunia siku ya Ijumaa, aliripotiwa kuwa kwenye lishe ya kioevu au majimaji kwa siku 14 - kujaribu kupunguza uzito haraka.

Siku chache kabla ya kifo chake, aliandika ujumbe kwenye mtandao wa Twitter akaweka picha yake ya zamani, akisema: "Lengo ifikapo Julai ni kurejea katika sura hii ya miaka michache iliyopita."

Marafiki wamesema ni hatua ambayo alikuwa ameijaribu mara kadhaa hapo awali.

Kwa hivyo vyakula hivi ni salama vipi na athari zake kwa mwili ni nini?

Kuna aina nyingi tofauti za lishe ya kioevu au majimaji lakini zote zina lengo sawa - kupunguza uzito haraka kwa kula kalori chache.

Zinatofautiana kutoka kwa vinywaji vya matunda vya mtindo mbalimbali na juisi za mboga mboga ambazo huelezwa kuondoa sumu na kusafisha mwili hadi zile zenye kalori ya chini na supu.

Lakini wataalam wanaonya mlo huu uliokithiri huwa na hatari za kiafya na haufai kwa watu wengi.

Wizara ya afya Uingereza inapendekeza lishe yake ya kalori 800 kwa siku kwa makundi fulani pekee, haswa watu wanene au wanene kupita kiasi wanaodhibiti kisukari cha aina ya 2.

Imejaribiwa na kufanyiwa majaribio, inawezekana kwa usaidizi mwingi na usimamizi wa kimatibabu - lakini ni nadra kuwa hivyo kwa vyakula vingine vya kioevu au majimaji vinavyopatikana mtandaoni.

"Milo ya juisi inawavutia watu kwa sababu wanataka mabailiko ya haraka - lakini kudhibiti mwili kwa ulaji chakula ni jambo gumu sana," Aisling Pigott, wa Shirika la Chakula la Uingereza, anasema.

"Inahusu wakati vyakula hivyo vinauzwa kwa watu ambao wana uzito mzuri."

Ruka Twitter ujumbe, 1

Mwisho wa Twitter ujumbe, 1

Juisi ya matunda na mboga mboga hutoa madini na vitamini nyingi - lakini protini au mafuta kidogo sana.

"Utahisi kuishiwa nguvu na uchovu baada ya wiki, " Dk Gail Rees, profesa msaidizi wa lishe ya binadamu, katika Chuo Kikuu cha Plymouth, anasema.

Mlo usio na uwiano wa lishe hauupi mwili kila kitu unachohitaji - na "unaweza kuwa wenye kuharibu zaidi" katika kipindi cha muda mrefu.

Akiba ya chuma ingetumika, ambayo inaweza kusababisha upungufu wa damu kwa wanawake, unene wa misuli ungepungua na utumbo, mapafu na ini vingelazimika kufanya kazi kwa nguvu zaidi ili kuufanya mwili kufanya kazi kwa kawaida.

Madhara mengine yanayoweza kutokea ni pamoja na maumivu ya kichwa, kizunguzungu, uchovu mwingi, kuhara au kuvimbiwa.

Juisi za matunda, ambazo zina asidi nyingi za asili, zinaweza pia kuharibu enameli kwenye meno na ukosefu wa ulaji wa kalori unaweza kufanya pumzi iwe tofauti.

Kupunguza uzito haraka kunawezekana kwenye lishe ya kioevu lakini changamoto kubwa, kulingana na Bi Pigott, ni "hatari" - hatari ya kurundika uzito tena wakati ulaji wa chakula unarudi kawaida.

Woman on a liquid diet

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Lishe zenye mafuta mengi ni "sehemu ya utamaduni wa lishe yenye sumu" inayohimiza mitazamo hasi kwa chakula na mara nyingi husababisha kuongezeka kwa uzito sio kupungua, anasema.

Na anapendekeza kusikiliza mwili wako mwenyewe, kurudi kwenye misingi na kuweka malengo yanayoweza kufikiwa ambayo yanafanya kazi kwa muda mrefu, sio tu kwa wiki.

'Kupunguza uzito kwa kuendesha baiskeli'

"Mlo uliokithiri sio suluhisho endelevu la kupunguza uzito kwa muda mrefu, kwani uzito mkubwa unaopotea unaweza kuwa maji au misuli iliyokonda," Dk Simon Steenson, wa mfuko wa Lishe wa Uingereza, anasema.

"Kutaka kupunguza mwili kwa haraka pia kunaweza kusababisha hatari za kiafya, kama vile hatari kubwa ya kupata mawe kwenye nyongo."

Dk Steenson pia anaonya juu ya "kuendesha baiskeli kwa nia ya kupunguza uzani"- mtindo wa kupunguza na kurejesha uzito kwa lishe ya mtindo huu - inaweza kuwa na athari mbaya za kiafya yenyewe.

Chaguo bora la kupunguza uzito, anasema, ni kulenga mlo tofauti na uwiano, ikiwa ni pamoja na matunda mengi, mboga mboga, nafaka nzima, maharagwe, karanga na mbegu, pamoja na kutafuta njia za kujishughulisha na kazi siku nzima.

Dk Rees anapendekeza kuachana na pombe, kaukau, biskuti na vyakula vya kununua vilivyopikwa kabisa ambavyo vyote vinatoa kalori zisizohitajika, badala ya kuzingatia upunguzaji uzito ndani ya kipindi kifupi "mlo wa kioevu au majimaji".

Na ikiwa una tatizo lolote la kiafya, wasiliana na daktari kila wakati au mtaalamu wa lishe kabla ya kuanza lishe.

Ikifanywa kwa njia sahihi, kwa watu wanaofaa, lishe ya kioevu inaweza kufanya kazi - lakini kwa watu wengi, ni ngumu sana kufuata na inaweza kuwa hatari isiyo ya lazima.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here