Je, mtandao wa barabara zinazovuka kote Kenya umekuwa mitego ya vifo? Kati ya 2020 na 2021 vifo vya ajali za barabarani nchini Kenya viliongezeka zaidi ya asilimia 20.
Mwaka jana, zaidi ya 4500 waliuawa na zaidi ya 16,000 kujeruhiwa.
Serikali ya Kenya inasema watu kuendesha magari wakiwa walevi , kupakia mizigo kupita kiasi, na mwendo kasi ni miongoni mwa sababu kuu za mauaji hayo.
Lakini je, rushwa nayo ni sababu? Mwandishi wa habari Richard Chacha, aliyepooza katika ajali ya barabarani miaka kumi iliyopita, anaungana na Africa Eye kuwafichua wafanyikazi wa shule ya udereva ambaohuwawezesha madereva ambao hawajahitimu kuendesha magari bila kulazimika kufanya mtihani wa udereva.
Africa Eye pia inafichua jinsi madalali wanavyochukua pesa kuupiku mfumo wa kupima usalama wa magari, kuwezesha teksi zinazofaa kwa rundo la vyuma chakavu kuendeshwa kwenye barabara za Kenya…na kubeba abiria.
No comments:
Post a Comment