MAYELE HATARI YAKE KILA DAKIKA 100 - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Wednesday 9 March 2022

MAYELE HATARI YAKE KILA DAKIKA 100

 

KINARA wa utupiaji wa mabao ndani ya kikosi cha Yanga, Fiston Mayele ana wastani wa kuwa na hatari kila baada ya dakika 100 awapo uwanjani kwenye kutupia pamoja na kutengeneza nafasi za mabao.

Ndani ya Ligi Kuu Bara ameyeyusha dakika 1,301 akiwa amefunga mabao 10 na ni mabao matano ametupia Uwanja wa Mkapa huku mabao matano ametupia nje ya Uwanja wa Mkapa.

Bao lake la kwanza alifunga Uwanja wa Majimaji, Songea mbele ya KMC na bao la 10 alifunga mbele ya Geita Gold Uwanja wa CCM Kirumba.

Ana hatari kila baada ya dakika 100 kwa kuwa amehusika katika mabao 13 ya Yanga akiwa ametoa pasi 3 za mabao.

Mchezo dhidi ya Geita Gold ambao ni wa mzunguko wa pili aliweza kufunga bao lake la mapema zaidi ikiwa ni dakika ya kwanza na lilikuwa ni bao pekee la ushindi.

Alitumia dakika 70 na nafasi yake ni Heritier Makambo aliweza kuichukua baada ya yeye kuumia lakini kwa sasa anaendelea vizuri.

Makambo alitumia dakika 20 kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here