Meli iliyopotea kupatikana baada ya miaka 107 - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Sunday 13 March 2022

Meli iliyopotea kupatikana baada ya miaka 107

 

Wheel

CHANZO CHA PICHA,FMHT/NATIONAL GEOGRAPHIC

Wanasayansi wameipata na kurekodi mabaki ya meli ambayo ni mojawapo ya ajali kubwa zaidi ambazo hazijawahi kugunduliwa miaka 107 baada ya kuzama.

Endurance, meli iliyopotea ya mpelelezi wa Antarctic ,Ernest Shackleton, ilipatikana mwishoni mwa juma chini ya Bahari ya Weddell.

Meli hiyo ilivunjwa na barafu ya baharini na kuzama mwaka wa 1915, na hivyo kumlazimisha Shackleton na watu wake kutoroka kwa njia ya kushangaza kwa miguu na kwa mashua ndogo.

Video ya mabaki inaonesha Endurance kuwa katika hali ya kushangaza.

Ingawa imekuwa ikikaa ndani ya kilomita 3 (futi 10,000) za maji kwa zaidi ya karne moja, inaonekana kama ilivyokuwa siku ya Novemba iliposhuka.

Mbao zake, ingawa zimevurugika, bado ziko sawa, na jina - Endurance - linaonekana vizuri.

"Bila kutia chumvi yoyote hii ndiyo meli nzuri zaidi ya mbao ambayo nimewahi kuona - hadi sasa," alisema mwanaakiolojia wa baharini Mensun Bound, ambaye yuko kwenye msafara wa ugunduzi na sasa ametimiza ndoto yake kubwa katika kazi yake ya karibu miaka 50.

"Iko vizuri, inajivunia chini ya bahari, haijabadilika, na iko katika hali nzuri ya uhifadhi," aliiambia BBC News.

Endurance

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES/SPRI

Maelezo ya picha,

Meli ya Endurance ilizama kwenye barafu kwa miezi kadhaa kabla ya kuzama kwenye kina kirefu 1915

Mradi wa kutafuta meli iliyopotea uliwekwa na Falklands Maritime Heritage Trust (FMHT), kwa kutumia meli ya kuvunja barafu ya Afrika Kusini, Agulhas II, na ikiwa na vifaa vya chini vya maji vinavyoendeshwa kwa mbali.

Kiongozi wa mpango huo, mwanajiografia mkongwe Dr John Shears, alielezea wakati kamera zilipotua kwenye jina la meli kama "kudondosha taya".

"Ugunduzi wa meli hiyo ni mafanikio ya ajabu," aliongeza.

"Tumefanikiwa kukamilisha utafutaji mgumu zaidi duniani wa ajali ya meli, tukipambana kila mara na barafu ya baharini, vimbunga, na halijoto kushuka hadi -18C. Tumefanikiwa kile ambacho watu wengi walisema hakiwezekani."

Agulhas

CHANZO CHA PICHA,FMHT AND NATIONAL GEOGRAPHIC

Meli ilipatikana wapi?

Endurance ilionekana katika Bahari ya Weddell katika kina cha 3,008m.

Kwa zaidi ya wiki mbili, wasaidizi hao walikuwa wametafuta eneo hilo ambalo walikuwa wanafanyia utafiti katika masuala mbalimbali waliyokuwa wameyalenga.

kabla ya kufichua eneo la meli siku ya Jumamosi - kumbukumbu ya miaka 100 ya mazishi ya Shackleton.

Siku kadhaa tangu ugunduzi huo umetumika kutengeneza rekodi ya kina za picha za mbao na mazingira yanayoizunguka.

Meli yenye iliyopata ajali ni mnara ulioteuliwa chini ya Mkataba wa kimataifa wa Antaktika na haupaswi kusumbuliwa kwa njia yoyote. Kwa hivyo hakuna vitu vya asili vilivyoletwa.

Watumiaji wanaweza kuona nini?

Meli inaonekana sawa na wakati ilipigwa picha kwa mara ya mwisho na mtengenezaji wa filamu wa Shackleton, Frank Hurley, mwaka 1915.

Baadhi ya uharibifu unaonekana kwenye upinde, labda mahali ambapo meli inayoshuka ilipiga chini ya bahari. Nanga zipo.

"Unaweza hata kuona jina la meli - ENDURANCE - Na yenye maandishi makubwa ya rangi ya shaba, na kuekwa nyota tano, baada ya meli hiyo kupewa jina," Mensun Bound alisema.

"Nakwambia, itabidi utengenezwe kwa jiwe ili ikae sawa mbele ya nyota huyo na jina hapo juu," aliongeza.

"Unaweza kuona dirisha dogo meli hii ya Shackleton Wakati huo, wewe ulijihi pumzi za mtu mashuhuri nyuma ya shingo yako."

Wheel

CHANZO CHA PICHA,FMHT/NATIONAL GEOGRAPHIC

Ni maisha gani yalikuwa yameunganishwa na meli?

Inafurahisha, meli hiyo imetawaliwa na maisha mengi - lakini sio ya aina ambayo ingeweza kutumika kwa sasa.

"Inaonekana kuwa kuna uchakavu mdogo wa mbao , ikimaanisha kwamba wanyama wanaopatikana katika maeneo mengine ya bahari yetu, labda haishangazi, hawako katika eneo lisilo na misitu la Antarctic," alitoa maoni mwanabiolojia wa polar ya kina kirefu Dkt Michelle Taylor kutoka. Chuo Kikuu cha Essex.

"Endurance, inayoonekana kama meli ya kishetani, imenyunyizwa na aina nyingi za kuvutia za viumbe vya baharini vya kina kirefu - za baharini, sponge za aina mbalimbali, na vitu vingine kutoka kina kirefu cha maji ya Bahari ya Weddell."

Wreck

CHANZO CHA PICHA,SPRI/UNI OF CAMBRIDGE

Maelezo ya picha,

Shackleton (kushoto) akiangalia masalio ya meli hiyo kabla haijazama

Kwa nini meli hii ilithaminiwa sana?

Kuna sababu mbili.

Ya kwanza ni hadithi ya Msafara wa Shackleton wa Imperial Trans-Antarctic

Ilianza kuvuka nchi ya kwanza ya Antaktika, lakini ilibidi kuachana na safari hiyo wakati meli ya msafara, Endurance, iliponaswa na kisha kufungwa na barafu ya baharini.

Kuanzia hapo ilikuwa ni jinsi ya kuishi. Kwa namna fulani Shackleton alifaulu kuwapeleka watu wake mahali salama, njia ya kutoroka ambayo ilimwona mvumbuzi wa Anglo-Irish mwenyewe akichukua mashua ndogo ya kuokoa maisha yake kuvuka bahari ili kupata usaidizi.

Sababu nyingine ilikuwa changamoto yenyewe ya kutafuta meli.

Bahari ya Weddell imefunikwa kabisa na barafu nene ya baharini, barafu ile ile ya bahari iliyopasua meli ya Endurance.

Kukaribia eneo linalodhaniwa kuwa la kuzama ni ngumu sana , ni suala gumu ukiachilia mbali suala la utafutaji.

Lakini hapa pia kuna sehemu ya mafanikio ya mradi wa FMHT. Mwezi uliopita umeshuhudia kiwango cha chini kabisa cha barafu ya bahari ya Antarctic kuwahi kurekodiwa wakati wa enzi ya satelaiti, ambayo inaanzia miaka ya 1970.

Hali zilikuwa nzuri bila kutarajia.

Sabertooth sub

CHANZO CHA PICHA,FMHT/NATIONAL GEOGRAPHIC

Agulhas walimaliza uchunguzi wa ajali hiyo na kuondoka eneo la utafutaji Jumanne.

Meli hiyo ya kuvunja barafu inaelekea bandari yake ya nyumbani ya Cape Town. Lakini nia ni kuiita katika Jimbo la Overseas la Uingereza la Georgia Kusini ambako Shackleton amezikwa.

"Tutatoa heshima zetu kwa 'The Boss'," Dk Shears alisema, akitumia jina la utani la kikundi cha Endurance kwa kiongozi wao.

Shackleton

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Bosi alizikwa kituo cha Grytviken Whaling huko South Georgia

Endurance

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here