Diana Bundala maarufu kama 'Mfalme Zumaridi' akiwa amejifunika kitenge ndani ya chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza kwa ajili ya kusomewa hoja za awali za mashtaka matatu yanayowakabili na wenzake. Picha na Mgongo Kaitira
Mwanza. Diana Bundala maarufu kama 'Mfalme Zumaridi' na wenzake 84 leo Alhamisi Machi 17, 2022 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza kusomewa maelezo ya awali katika mashtaka matatu ikiwamo usafirishaji haramu wa binadamu.
Makosa mengine ni pamoja na kusanyiko lisilo na kibali na kuzuia maofisa wa Serikali kutimiza wajibu wao.
Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo saa 6:00 mchana mbele ya ya Hakimu mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo, Monica Ndyekubora.
Huyu ndiyo ‘Mfalme Zumaridi’
Kwa miaka kadhaa sasa, ‘Mfalme Zumaridi’ ambaye jina lake halisi ni Diana Bundala, ni miongoni mwa wahubiri wa dini wanaovuma ndani na nje ya Jiji la Mwanza. Soma zaidi
No comments:
Post a Comment