MWAKA MMOJA WA KIFO CHA MAGUFULI KUKUMBUKWA KWA VITENDO - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Wednesday 16 March 2022

MWAKA MMOJA WA KIFO CHA MAGUFULI KUKUMBUKWA KWA VITENDO

 

UONGOZI wa Yanga umebainisha kwamba utaenzi kwa vitendo mwaka mmoja wa kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati John Pombe Magufuli.

Klabu ya Yanga imekuwa na utamaduni wa kutoa kwa jamii ambapo wiki iliyopita ilicheza mechi ya hisani kwa ajili ya kuchangia Taasisi ya Ally Kimara na mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 1-1 Timu ya Taifa ya Somalia ambapo ni milioni 41 zimetajwa kwamba zilikusanywa katika mchezo huo.

Leo Machi 17, ikiwa ni mwaka mmoja umetimia tangu Rais Magufuli afariki ambapo Yanga wamepanga kwenda Hospital ya Ocean Road kutoa msaada.

Pia wamepanga kusherehekea mwaka mmoja wa uongozi wa Awamu ya Sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Samia Hassan Suluhu kwa kuchangia damu Hospital ya Muhimbili.

Pia Yanga wameweka wazi kwamba wamemuomba Rais Samia kuhudhuria mchezo wa Ligi Kuu Bara Jumamosi dhidibya KMC, Uwanja wa Mkapa akiwa kama mgeni rasmi.

Haji Manara,Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa katika tukio la kumkumbuka Rais Magufuli Wanayanga leo watakwenda kutoa msaada katika Hospital ya Ocean Road.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here