Mwanafunzi wa Afrika Kusini aliyetumia dola milioni moja alizopokea kimakosa ahukumiwa miaka mitano jela - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Thursday, 31 March 2022

Mwanafunzi wa Afrika Kusini aliyetumia dola milioni moja alizopokea kimakosa ahukumiwa miaka mitano jela

 

th

Mwanamke mmoja wa Afrika Kusini ambaye alifanya matumizi makubwa baada ya kupokea kimakosa karibu $1m (£700,000) katika akaunti yake ya benki amefungwa jela miaka mitano.

Sibongile Mani alipokea randi 14m badala ya 1,400 alizostahili kupata 2017 na kuanza kuzitumia mara moja, mahakama ilisikiza wakati wa kesi yake.

Pesa hizo zilitoka kwa Mpango wa Kitaifa wa Msaada wa Kifedha kwa Wanafunzi (NSFAS) kupitia kampuni ya huduma za malipo, Intellimali, alipokuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Walter Sisulu. Lakini hakuripoti kosa hilo.

Badala yake, alianza kutumia pesa hizo ndani ya masaa mawili baada ya kuzipokea

Kufikia wakati akaunti yake ilipozuiwa, alikuwa ametumia karibu $70,000 katika maeneo 48 kote nchini kwa siku 73.

Alitumia pesa hizo kununua nywele bandia, simu za rununu, pombe, godoro, kadi za zawadi na bidhaa za kifahari miongoni mwa zingine.

Katika kumhukumu, mahakama ilibaini kuwa ilikuwa ya kushangaza kwamba alikuwa ameweza kutumia pesa nyingi kwa siku kote nchini.

Ilisema kuwa wanafunzi wengi wangeathirika kama Intellimali, kampuni iliyosambaza fedha za NSFAS, isingelipa pesa alizotumia.

Jaji pia alibainisha kuwa matumizi yake yalichochewa na "uchoyo", akitupilia mbali hoja kwamba alikuwa mwathirika wa maisha duni.

Alipatikana na hatia ya wizi na alihukumiwa jela siku ya Jumatano.

Wakili wake amesema watakata rufaa dhidi ya hukumu hiyo na hukumu itakayosikilizwa tarehe 11 Aprili.

Kesi hiyo imezua maoni tofauti, huku wengine wakiona alichokifanya kuwa halali katika nchi ambayo mengi zaidi yanapotea kupitia ufisadi miongoni mwa maafisa wa umma.

Wengine, hata hivyo, wanaona hii kama haki imetendeka.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here