Mwanamke wa Ukraine aliyepigwa risasi na askari wa Urusi - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Wednesday, 30 March 2022

Mwanamke wa Ukraine aliyepigwa risasi na askari wa Urusi

 

Natalia Mykolaivna

CHANZO CHA PICHA,BBC NEWS

Maelezo ya picha,

Natalia anasumuka na majeraha kadhaa

Urusi imesema hailengi raia - majengo wanamoishi na kufanyia kazi, au watu wenyewe.

Akiwa amelazwa katika kitanda cha hospitali katika mji wa kusini mwa Ukraine wa Zaporizhzhia, Natalia Mykolaivna anadhihaki kukanusha huko kwa Warusi.

Hadi wiki ya pili ya mwezi Machi, Umoja wa Mataifa ulisema kwamba mashambulizi ya Urusi dhidi ya malengo ya raia nchini Ukraine yanaweza kuwa uhalifu wa kivita.

Tangu wakati huo kumekuwa na mashambulizi mengi, yaliyoandikwa ambapo raia wamekufa kwa wingi - ikiwa ni matokeo ya mashambulizi ya kiholela na mazito ya maeneo ya raia.

Lakini kile kilichotokea kwa Natalia mwenye umri wa miaka 45 kilikuwa cha makusudi, kilicholengwa na bila uhalali.

Ni muujiza kwamba bado yuko hai.

Akiwa ameshika mkono wa mwanawe, Nikolai, aliniambia yaliyotokea katika mji wa kwao wa Polohy siku ambayo majeshi ya Urusi walipowasili.

"Nilitoka nyumbani kwangu, nilikuwa namuhofia mama yangu , nikaenda kumuona.

Alikuwa akiishi mtaa wa karibu na kwetu," alisema Natalia, ambaye alielezea jinsi alivyoruhusiwa kupita katika kituo cha kwanza cha ukaguzi cha jeshi la Urusi.

"Kisha nilitembea kuelekea nyumbani kwa mama yangu, nikainua mikono yangu hewani - nikisema tayari nimeambiwa naweza kupita - lakini askari huyo alinifyatulia risasi kuanzia kwenye miguu, kila mahali kutoka kiunoni kwenda chini. "

Natalia hakuwaona sura zao wala kusikia sauti ya yule askari wa kirusi aliyempiga risasi.

"Hakusema neno. Walikuwa wamesimama karibu na tanki lenye herufi Z", aliendelea. "Wote walikuwa wamevaa barakoa au vinyago."

Natalia alihamishwa na majirani na familia yake hadi hospitali iliyo karibu na Zaporizhzhia na tangu wakati huo ameambiwa na madaktari kwamba alinusurika kifo "kwa milimita moja".

"Madaktari hawataniambia ni risasi ngapi. Nilipigwa risasi kutoka kiunoni kwenda chini," alisema huku akinionesha jeraha la risasi tumboni mwake. "Kuna moja hapa, na hapa na hapa pia. Kila kitu kimeharibika, sehemu zangu za siri pia."

Orikhiv market

CHANZO CHA PICHA,BBC NEWS

Mguu wa kulia wa Natalia umevunjika, unashikiliwa na chuma. Goti lake limevunjwa kabisa na hatatembea tena kama alivyokuwa akitembea awali.

Polohy, kijiji ambacho sasa kinakaliwa ambapo Natalia alipigwa risasi, kiko barabarani kuelekea mji uliozingirwa wa Mairupol. Ni kilomita chache tu kusini mwa Orikhiv, kijiji kidogo cha wakulima.

Orikhiv ndicho kijiji cha mwisho kinachoshikiliwa.

Watu wengi, haswa familia za vijana, wameondoka kwa usalama wa jamaa wa Zaphorizhzhia au miji ya magharibi zaidi.

Lakini wakazi wengi wazee, madaktari na walinzi wa raia walibaki.

Lida Vasylivna

CHANZO CHA PICHA,BBC NEWS

Maelezo ya picha,

Lida alikuwa anaishi Orikhiv

Shamba dogo la kisasa la Lida Vasylivna, liko kwenye ukingo wa Orikhiv - sehemu iliyo wazi zaidi na hatari katika jiji.

Tunapokutana naye, Lida anafanya kazi kwa bidii katika sehemu ya mboga, kupanda viazi na kupanda mbegu - kuchukua fursa ya hali ya hewa baada ya baridi kali.

Anapofunika mbegu za viazi zilizoachwa wazi , sauti ya makombora ya Kirusi inaweza kusikika kwa mbali.

Watoto wa Lida na mume wake mgonjwa, ambaye amepatwa na kiharusi mara mbili tangu kuanza kwa vita, wako salama, maili chache kutoka katika makazi ya jumuiya.

Lakini anabaki, akichunga mazao yake na wanyama wake - ikiwa ni pamoja na kondoo na sungura. Lida anajivunia ukweli kwamba karibu anajitosheleza kabisa kwa chakula, na amedhamiria kutopoteza kila kitu alichojenga.

Lida anaishi katika nyumba ya kawaida. Lakini hawezi kulala huko - ni hatari sana. Kwa hivyo, anatuonesha mahali anapolala - nje, kwenye sehemu ya baridi na unyevunyevu ambapo kwa kawaida angeweka viazi na kachumbari zake wakati wa majira ya baridi. Miongoni mwa zana za mazao na bustani kuna godoro na mto.

"Nimejificha kwenye chumba hiki cha kulala kwa sababu wanatupiga kwa mabomu na kushambulia kutoka kila upande, Lida alisema kwa machozi. "Ninawachukia, ninawachukia ... Tulikuwa tunaishi kwa amani, na tulikuwa na furaha.

Locals take a course in a hospital

CHANZO CHA PICHA,BBC NEWS

Katika mji mdogo, ambapo vita ni jambo geni lisilokubalika - kila mtu ambaye ameamua kukaa anabadilika na kujifunza haraka.

Madaktari kutoka hospitali ndogo ya Orikhiv, wauguzi na wasaidizi wa dharura wamepewa mafunzo ya kukabiliana na kiwewe na kutoa huduma wakati wa vita.

Wana nia ya kujifunza lakini wanajua jinsi isivyokuwa rahisi.

"Ni majaribio ya kimsingi lakini katika hali ya majeruhi," alisema Guillaume Barreau, mkufunzi wa mafunzo kutoka Medecins Sans Frontiers.

Akifanya kazi karibu na giza kwa sababu ya kukatwa kwa umeme kwa muda mrefu katika mji, Barreau alisema madaktari hawa wanapaswa kujifunza kutoa huduma ambazo hawakupata mafunzo yake. "Wanahitaji kujua jinsi ya kuzingatia wagonjwa wanaoweza kuokolewa. Kila mtu anajua kwamba ikiwa hii itatokea, hutokea wakati ambao haukutarajiwa."

Muda mfupi baada ya kuondoka Orikhiv, tulipigiwa simu na Lida. Kulikuwa tu na shambulio kubwa.

Hakukuwa na majeruhi yoyote.

Akitikiswa, lakini akiwa amedhamiria, Lila alikaa na kukaa usiku kucha katika makazi yake.

Mengi zaidi

line

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here