Wakati Vladimir Putin alipovunja amani huko Ulaya kwa kuanzisha vita juu ya demokrasia ya watu milioni 44, alihalalisha hilo kwa kusema kwamba Ukraine ya kisasa, inayofuata umagharibi ilikuwa tishio na Urusi haikuweza kujiona iko "salama, kuendelea na kuwepo".
Lakini baada ya wiki kadhaa za mashambulizi ya mabomu, kumesababisha maelfu ya vifo na msururu wa mamilioni ya wakimbizi, swali linabaki: lengo lake la vita ni nini na kuna njia yoyote ya kujinasua?
Nini anachokitaka Putin?
Lengo la awali la kiongozi huyo wa Urusi lilikuwa ni kuipindua Ukraine na kuiangamiza serikali yake, na kuzima nia yake njema ya kujiunga na muungano wa kujihami wa nchi za Magharibi, NATO.
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Aliwaambia watu wa Urusi kuwa lengo lake lilikuwa "kuiangamiza na kuiangamiza Ukraine", kuwalinda watu walio chini ya kile alichokiita miaka minane ya unyanyasaji na mauaji ya kimbari yaliyofanywa na serikali ya Ukraine. "Sio mpango wetu wa kulikalia eneo la Ukraine. Hatuna nia ya kulazimisha kitu chochote kwa nguvu," alisisitiza.Lakini hakukuwa na Wanazi na hakuna mauaji ya kimbari, na Urusi imesambaza vikosi vyake vya jeshi katika miji kadhaa huku raia wa Ukraine wakipinga uwepo wake.
Mashambulizi ya mabomu yanaendelea - lakini ripoti za hivi karibuni kutoka kwa mazungumzo ya amani zinaonyesha kuwa Urusi haitaki tena kuipindua serikali na badala yake inalenga kuwepo kwa Ukraine isiyoegemea upande wowote.
Kwa nini Putin anataka Ukraine isiyoegemea upande wowote
Tangu Ukraine ilipopata uhuru wake mwaka 1991, wakati Umoja wa Kisovyeti ulianguka, ikabadili muelekeo na hatua kwa hatua kuwa washirika wa - Umoja wa Ulaya EU na Nato.
Kiongozi wa Urusi anakusudia kubadili hilo, akiona kuanguka kwa Umoja wa Kisovyeti kama "kuvunjika kwa historia ya Urusi".
Alidai raiawa wa Urusi na Ukraine ni wamoja. "Ukraine haijawahi kuwa na utamaduni wa utaifa wake," alisema, akipinga historia ya Ukraine.
Mwaka 2013 alimshinikiza kiongozi wa Ukraine anayeungwa mkono na Urusi, Viktor Yanukovych, kutotia saini makubaliano na Umoja wa Ulaya, na kusababisha maandamano ambayo hatimaye yalimuondoa madarakani kiongozi huyo wa Ukraine mwezi Februari 2014.
Urusi ililipiza kisasi mwaka 2014 kwa kuliteka eneo la kusini mwa Crimea la Ukraine na kusababisha uasi mashariki, ikiunga mkono waasi ambao walipigana na vikosi vya Ukraine katika vita vya miaka minane ambavyo vilisababisha vifo vya watu 14,000.
Kulikuwa na usitishaji mapigano, na mkataba wa amani wa Minsk wa 2015 ambao haukutekelezwa.
Kabla ya uvamizi wake, Rais Putin alivunja makubaliano ya amani na kutambua mataifa mawili yanayoungwa mkono na Urusi kama mataifa huru nje Ukraine.
Alipokuwa anatuma wanajeshi wake huko, aliishutumu Nato kwa kutishia "mustakabali wetu wa kihistoria kama taifa", akidai bila ya uthibitisho kwamba nchi za Nato zilitaka kuleta vita Crimea.
Je, kuna njia ya kuondokana na vita hivi?
Mshauri wa rais wa Ukraine Mykhailo Podolyak anaamini usitishaji mapigano unaweza kuanza katika siku zijazo kwa sababu vikosi vya Urusi vimekwama kusonga mbele kwenye vita hiyo.
Pande zote mbili zinasema mazungumzo yanaendelea vizuri katika mazungumzo, na Podolyak anasema rais wa Urusi amelegeza matakwa yake.
Mwanzoni mwa vita, kiongozi huyo wa Urusi alitaka Ukraine kuitambua Crimea kama sehemu ya Urusi na kutambua uhuru wa upande wa mashariki unaoendeshwa na waasi. Ukraine italazimika pia kubadilisha katiba yake ili kuhakikisha kuwa haitajiunga na Nato na Eu.
Mustakabali wa baadaye wa Crimea na majimbo yanayoungwa mkono na Urusi huko Luhansk na Donetsk bado haujapata utatuzi, lakini huenda wasiwe wavunjaji wa makubaliano ikiwa pande hizo mbili zitakubaliana kushughulikia suala hilo baadaye.
Urusi inaonekana kukubali kuwa haiwezi kuuondoa uongozi wa Ukraine na kuweka serikali kibaraka kama ilivyo Belarus. Rais Volodymyr Zelensky alisema mwanzoni mwa vita alikuwa alionywa kuwa "adui (Putin) ameniteua mie kama mlengwa namba moja; Familia yangu ni mlengwa namba mbili."
"Inaonekana kama [Putin] atalazimika kukubali masuala kidogo zaidi," anasema Tatiana Stanovaya, wa kampuni ya uchambuzi ya RPolitik na Kituo cha Carnegie Moscow.
Hiyo ni kwa sababu Urusi inafikiria "Ukraine isiyoegemea upande wowote na isiyokuwa na vikosi vingine" ibaki la jeshi lake lenyewe (la Ukraine), kama ilivyo kwa Austria au Sweden, ambao wote ni wanachama wa EU. Austria haiegemei upande wowote, lakini Sweden haiko hivyo. Imejiweka kando na masuala ya Nato.
Nini mahitaji ya Ukraine?
Mahitaji ya Ukraine yako wazi, anasema mshauri wa rais: kusitisha mapigano na uondoaji wa majeshi ya Urusi, lakini pia kuingia makubaliano ya kisheria ya amani ambayo yataihakikisha usalama Ukraine na kupata ulinzi kutoka kundi la nchi washirika ambalo litashiriki kikamilifu kuzuia mashambulizi na "kuwajibika kutatua mzozo huko Ukraine".
Ukraine pia imepunguza msimamo wake tangu ivamiwe na Urusi, Rais Zelensky akisema kuwa Ukraine sasa inaelewa kwamba Nato haitakubali Ukraine kuwa mwanachama: "Ni ukweli na lazima ufahamike."
"Tunafanyia kazi nyaraka ambazo marais wataweza kuzipitia kujadili zaidi na kutia saini. Ni wazi hii linakuja sasa tena kwa haraka kwa sababu hii ndiyo njia pekee ya kumaliza vita hivi," Podolyak aliiambia televisheni ya Marekani PBS.
No comments:
Post a Comment