HII picha imepigwa hivi karibuni Ngorongoro Crater katika eneo la Ngoitok tok picnic site (eneo la kulia chakula), moja katika maeneo pendwa kabisa kwa watalii kwenye Crater yetu.
Ngoitok tok ni moja kati ya maeneo ambayo maji hayakauki throughout the year ukienda kiangazi, masika maji hayakauki na ni Kwa sababu ni moja ya maeneo natural ambayo maji hayakauki, kuna bathroom safi na salama kwa watalii kula chakula, kupiga picha na kushuhudia wanyama kama Kiboko na Mamba huku wakifurahia uoto asili wa Ngorongoro yetu.
Ninachotaka kusema ni kwamba Rais wetu Samia Suluhu Hassan ameifungua Nchi haswa, hichi ni kipindi ambacho kwenye Utalii tunaita Low Season (kipindi cha uhaba wa watalii) lakini namba kubwa ya magari ya Utalii yamepaki kwenye eneo hili la Ngoitok tok hii inaonesha ni jinsi gani watalii ni wengi sasa hivi kulinganisha na nyakati zingine za mwezi Januari na Machi ambapo wageni huwa hafifu. Maana yake ikifika Juni na Julai nyakati za High Season wageni watakua wengi zaidi ya hawa.
Namna ambavyo Rais wetu anaendelea kufungua Nchi kimataifa ukiongeza na Royal Tour aliyofanya tuendelee kutegemea idadi kubwa ya wageni kumiminika kwenye hifadhi zetu.
Ukiacha Ngoitok tok ya Ngorongoro kwa upande wa Serengeti wageni ni wengi sana katika eneo la Ndutu kwa sababu ya migration ya wanyama aina ya Nyumbu na Pundamilia.
Nchi imefunguliwa na Rais Samia, Utalii umeshika kasi katika miezi hii ya Low Season, tuseme nini kwa Mama Samia?
Neno ni Moja tu, Mama endelea kufungua Nchi.
Ngoitok tok imefunguka, Ndutu Serengeti pamefunguka, Tarangire na Manyara pia wageni ni wengi.
Tunywe mtori nyama ziko chini. #Kazi Iendelee.
No comments:
Post a Comment