SIMBA KUKWEA PIA KUWAFUATA WAPINZANI WAO ASEC - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Thursday 17 March 2022

SIMBA KUKWEA PIA KUWAFUATA WAPINZANI WAO ASEC

 

IMEELEZWA kuwa kesho Ijumaa wawakilishi wa Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho, Simba wanatarajia kukwea pipa kueleka nchini Benini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Jumapili ya Machi 20,2022 ukiwa ni mchezo wa tano kwenye hatua ya makundi na unatarajiwa kuchezwa nchini Benin.

Kwenye Kundi D, Simba ni vinara wa kundi wakiwa na pointi 7 wanakutana na ASEC Mimosas ambao wapo nafasi ya pili na pointi zao ni 6.

Mchezo wao uliopita walipokutana Uwanja wa Mkapa, Simba ilishinda mabao 3-1 na bao la Pape Sakho kwa mtindo wa Acrobatic lilitajwa kuwa bao bora la wiki.

Miongoni mwa wachezaji ambao wamekuwa imara ndani ya mechi za kimataifa pia ni pamoja na beki Mohamed Hussein, Zimbwe ambaye ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Pablo Franco.

Taarifa kutoka ndani ya Simba zimeeleza kuwa kila kitu kinakwenda sawa na wanatarajia kuondoka mapema ili kuweza kwenda kuanza maandalizi.

“Maandalizi yapo vizuri na kila kitu kinakwenda sawa kikosi kinatarajia kuondoka kesho kwa ajili ya mchezo wetu ujao,”.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here