WAHAMIAJI HARAMU 55 WAMEKAMATWA KATAVI - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Tuesday, 29 March 2022

WAHAMIAJI HARAMU 55 WAMEKAMATWA KATAVI

 

Afisa uhamiaji mkoa wa Katavi Vicent Haule akizungumza na waandishi wa habari 

Baadhi ya wahamiaji haramu wakiwa nje ya Ofisi ya Uhamiaji mkoa wa Katavi

*********************

Zillipa Joseph, Katavi

Ofisi ya uhamiaji mkoa wa Katavi limewabaini wahamiaji haramu 55 raia wa Burundi walioingia nchini bila ya kufuata taratibu na kuendelea kufanya kazi za vibarua mashambani, huku wengine wakifanya kazi katika machimbo ya dhahabu na baadhi yao wakiwaingiza watoto wao kusoma katika shule mbalimbali za msingi

Akitoa taarifa ya zoezi linaloendelea la msako, doria na ukaguzi Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Vicent Haule ambaye pia ni afisa uhamiaji wa mkoa wa katavi amesema zoezi hilo limefanyika katika maeneo ya ikola, ruhafwe na mpanda

Kati yao raia hao wa burundi saba bado wanachunguzwa, 30 watarudishwa burundi wakiwemo akina mama na watoto na 15 watafikishwa mahakamani

Bwana Haule pia amewataja raia watatu wa burundi waliotoroka katika makazi ya wakimbizi yaliyopo ya nyarugusu na nduta mkoani kigoma ambao amesema watarudishwa katika kambi hizo

Ameongeza kuwa kumekuwa na wimbi kubwa la uingizaji wa watoto kutoka Burundi kwa ajili ya kuja kupata elimu bure ambapo katika msako huu wamekamata wanafunzi katika shule mbalimbali za msingi

Aidha ameonya juu ya tabia ya kukaribisha raia wa kigeni kwa ajili ya vibarua mbalimbali kama kutunza mifugo na mashamba

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here