Ili kuhakikisha uzinduzi wa mbio za mwenge utakaofanyika mkoani Njombe April 2 mwaka huu unafanikiwa.Waziri wa wizara ya vijana,habari,utamaduni na michezo kutoka Zanzibar Tabia Mwita amekagua na kuridhishwa na maandalizi ya zoezi hilo linaloendelea mkoani humo.
“Nimetembelea maeneo tofauti tofauti,nimewaona watotot wanaofanya mazoezi ya halaiki lakini pia kwenye uwanja.Kimsingi nimefarijika sana kuona wanafanya vizuri na watotot wameshaanza kuelewa kwa kufanya mazoezi vizuri”alisema Tabia Mwita
Aidha kwa upande wa uwanja utakaotumika kwa ajili ya zoezi la uzinduzi Mwita amesema ukarabati unakwenda vizuri.
“Ukarabati unakwenda vizuri na tumeendelea kushauri baadhi ya mambo kwa hiyo kimsingi nimefurahi kuwepo hapa na maandalizi karibuni 70% iko vizuri”
Vile vile ametoa wito kwa wadau kuendelea kuchangia shughuli hiyo ili iweze kufanikiwa zaidi.
Amesema serikali ya mapinduzi ya Zanzibar itatoa ushirikiano mkubwa ili kuhakikisha shughuli hiyo inafanyika vizuri.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa ameihakikishia serikali kuwa maandalizi yatakamilika kwa wakati ili kufanikisha shughuli hiyo.
“Tumejipanga vizuri na niwakaribishe wananchi wote waje Njombe siku hiyo ili waone namna tunavyowasha mwenge kitofauti”alisema Kissa Kasongwa
Waziri wa wizara ya vijana,habari,utamaduni na michezo kutoka Zanzibar Tabia Mwita na viongozi wengine wakitazama mazoezi ya watoto wa halaiki yanayofanyika katika uwanja wa shule ya sekondari Mpechi.
Waziri wa wizara ya vijana,habari,utamaduni na michezo kutoka Zanzibar Tabia Mwita akikagua uwanja wa Saba saba mjini Njombe utakaotumika kwa shughuli za uzinduzi wa mbio za mwenge.
No comments:
Post a Comment