hayo yamesemwa jana wakati wa Ibada ya Alhamisi ya Amri kwenye Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu Dodoma na Askofu wa Kanisa Anglikana Tanzania Dayosisi ya Central Tanganyika Rt. Rev. Dr. Dickson Chilongani (PhD)
Wakati wa Mahubiri yake Askofu Dr. Dickson Chilongani alisema Yesu alitoa Amri Kuu ambayo ni Upendo
Alitolea mfano wa jinsi Yesu alivyowapenda adui zake akiwemo Yuda iskariote aliyemsaliti lakini alimuonesha Upendo kwa kummegea Mkate wakati wa Chakula Cha mwisho.
Hata msalabani ingawa alikuwa ni MUNGU badala ya kuwahukumu adui zake yeye aliwasamehe.
Askofu Dr. Chilongani alisistiza sana kama Kanisa, Dayosisi, Wakristo na Familia kwa ujumla tupendane.
Kuhusu Kuosha miguu kwa wanafunzi wa Yesu ilikuwa ishara ya Yesu Kutumika na siyo kutumikiwa hivyo kama wafuasi wake lazima tuige hicho kielelezo tutumike siyo kutumikiwa.
Askofu Dr. Chilongani alipongeza mpango wa Idara ya Vijana Kanisa Kuu kwa kuandaa mpango wa kutoa Sadaka kwa kituo Cha Buigiri kusaidia watu wasioona na wenye Mahitaji maalumu.
Akasisitiza kuwa katika kipindi hiki tunapoadhimisha mateso, kifo na kufufuka kwa Yesu Kristo lazima tuwakumbuke Wengine na kujitoa kwa upendo katika kuwasaidia wote wenye uhitaji.
Idara ya Vijana Kanisa Kuu kwa kushirikiana na Wakristo wote wakiongozwa na Sub Dean Rev. Keneth Chimwaga wametoa vitu Mbalimbali kwa ajili ya kusaidia watu wenye Mahitaji maalumu katika Shule ya Buigiri
KUZALISHA FAIDA KWA KRISTO NA KANISA
MUNGU IBARIKI DCT

No comments:
Post a Comment