Kifo cha Osinachi Nwachukwu:Binti wa mhubiri wa kanisa la Dunamis azungumza kuhusu kifo cha Osinachi - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Tuesday, 12 April 2022

Kifo cha Osinachi Nwachukwu:Binti wa mhubiri wa kanisa la Dunamis azungumza kuhusu kifo cha Osinachi

 

th

CHANZO CHA PICHA,INSTAGRAM

"Sipati usingizi kwa sababu kwa siku chache zilizopita kwa ajili ya hasira yangu kutokana kwa na kuondoka kwa moja ya sauti za kipkee katika kizazi chetu."

Binti ya mchungaji wa Dunamis International Gospel Centre, Deborah Paul Eneche, amezungumza kuhusu hali iliyosababisha kifo cha mwimbaji wa nyimbo za Injili wa Nigeria, Osinachi Nwachukwu.

Kabla ya kifo chake, Osinachi alikuwa mwimbaji mkuu wa Dunamis International Gospel Centre.

Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka arobaini alifariki Ijumaa jijini Abuja kutokana na madai ya unyanyasaji wa nyumbani kutoka kwa mumewe, Peter Nwachukwu.

th

CHANZO CHA PICHA,PETER NWACHUKWU/FACEBOOK

Hapo awali, ripoti zinasema kwamba mwimbaji huyo aliga dunia akiwa hospitali moja alikolazwa kwa siku kadhaa .

Baada ya habari za kifo chake , wafanyakazi wenzake wengi na baadhi ya mashabiki kwenye mitandao ya kijamii walikuja kumshutumu mumewe wakisema alimpiga.

Eneche anasema Osinachi Nwachukwu ndiye aliyemtia moyo kumfuata Mungu.

"Siwezi kueleza jinsi nilivyopata mshtuko baada ya kusikia hivyo"

Anasema kwamba hakujui jinsi alivyokuwa akiishi kabla ya sasa (madai ya unyanyasaji wa nyumbani) na kwamba ni nadra sana kwake kujiingiza katika maisha ya mtu mwingine.

Binti ya mchungaji huyo anasema anatamani angeweza kuzungumza na mwimbaji huyo ili kufahamu alichokuwa akipitia .

"Natamani ningejua uchungu aliopata."

Wakati huo huo, Eneche anaahidi kufanya kila jambo analoweza kufanya, ili kujua kilichofanyika.

Pia anasema watu wengi walikuwa karibu na marehemu Nwachukwu kabla ya kifo chake na hawakuwa na ufahamu kabisa kuhusu kilichokuwa kikifanyika .

'Yeye alitengwa na wapendwa wake'

Binti yake mchungaji alisema mwimbaji huyo ambaye ni marehemu alitengwa na wapendwa wake na hangejipata katika matatizo hayo iwapo hangetengwa na wanaompenda'.

th

CHANZO CHA PICHA,PETER NWACHUKWU/FACEBOOK

"Anakufa akiwa amevunjika moyo na mimi binafsi ninajitahidi niwezavyo kuhakikisha kuwa aliyetenda kosa hilo anapata adhabu kwa mujibu wa sheria."

Pia anaahidi kuchukua hatua na kuwalinda watoto wake na familia yake pia.

Kanisa limesema nini kuhusu unyanyasaji wa nyumbani?

Eneche pia aliweka wazi juu ya mafundisho ya kanisa kuhusu unyanyasaji wa nyumbani.

"Baba yangu daima huwa mtetezi wa kujiondoa kutoka kwa ndoa isiyokuwa na amani'

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here