SERIKALI imesema imepanga kutengeneza Barabara ya Babati-Galapo hadi Orkesmet wilayani Simanjiro kwa kiwango cha lami fedha zitakapopatikana.
Akijibu swali la Daniel Sillo Mbunge wa Jimbo la Babati vijijini Bungeni jijini Dodoma leo April 8,2022, naibu waziri wa ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema barabara hiyo ni muhimu na tayari imeshafanyiwa ufanisi wa kina.
Mheshimiwa Sillo aliuliza “ni lini serikali itaanza kujenga bara bara ya Babati-Galapo hadi Orkesmet kwa kiwango cha lami”?
Kasekenya amesema serikali inaendela kutafuta fedha ili bara bara hiyo ianze kujengwa kwa kiwango cha lami.
“Mheshimiwa Spika mara baada ya serikali kupata fedha bara bara hiyo itaanza kujengwa kwa kiwango cha lami” alisema Naibu waziri.
Ujenzi wa miundombinu ya barabara hiyo kwa kiwango cha lami itafungua maeneo hayo kibiashara na kuchochea fursa nyingi za kimaendeleo katika mkoa wa Manyara kwa kuwawezesha wakulima kusafirisha mazao yao kirahisi.
Friday, 8 April 2022
SERIKALI KUTAFUTA FEDHA KUJENGA BARABARA YA BABATI GALAPO HADI ORKESMET
Tags
# KITAIFA
About kabatamaiko
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
Newer Article
HALMASHAURI YA MLELE YAANDIKISHA WANAFUNZI 1,915 WA DARASA LA AWALI
Older Article
UJENZI WA BARABARA YA IGAWA HADI TUNDUMA WAIVA
"Stori za Afya za Wanawake wa Tanzania zina thamani kwetu", Absa Bank
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Mwinyi Amewaapisha Makatibu Wakuu Aliyewateua Hivi Karibu
Mkurugenzi mshauri wa USAID afanya ziara kukagua miradi ya USAID Afya Yangu na Kizazi Hodari Kanda ya Kusini
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment