Barcelona imepeleka dau ili kutumia faida ya vikwazo ilivyowekewa Chelsea kwa kujaribu kuwasajili mabeki wake watatu waliowahi kushinda kombe la ligi ya mabingwa Ulaya Mjerumani Antonio Rudiger, 29, Mhispania Cesar Azpilicueta, 32, na Mdenmark Andreas Christensen, 25. (Telegraph - subscription required)
Manchester United inatarajia mshambuliaji wake mreno Cristiano Ronaldo, 37, ataondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu, akiwa ametumia nusu tu ya miaka miwili ya mkataba wake. (Football Insider)
Leicester City ina matumaini ya kumshawishi kiungo wa Ubelgiji Youri Tielemans, 24, kusaini mkataba mpya, licha ya kusakwa na vilabu vya Manchester United Arsenal. (Team Talk)
Kiungo Mbrazil Douglas Luiz, 23, anaweza kuondoka Aston Villa msimu huu, huku Meneja wa timu hiyo Steven Gerrard akiipa kipaumbele kikubwa nafasi ya kiungo mkabaji kwenye usajili wa msimu ujao. (Mail)
Everton inajiandaa kumsajili mlinzi wa kati wa Leicester City kutoka Denmark Jannik Vestergaard, 29. (Football Insider)
Beki ya kupanda ya Middlesbrough Djed Spence, anayecheza kwa mkopo Nottingham Forest, anataka kuhamia ligi kuu- huku Arsenal na Tottenham zikuhusishwa na uhamisho wake wa gharama ya £20m mwishoni mwa msimu. Manchester United pia inamtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa England chini ya miaka-21. (Mirror)
Leeds United wanamtaka mlinzi wa pembeni wa Barcelona na Marekani Sergino Dest, 21. (Team Talk)
Nottingham Forest inataka kubadili mkopo wa kiungo muingereza James Garner, 21 kutoka Manchester United kuwa usajili wa kudumu mwishoni mwa msimu, lakini hilo litategemea kama watafanikiwa kupanda daraja kucheza ligi kuu England. (Football Transfers)
RB Leipzig wanajiandaa kufanya mazungumzo ya mkataba mpya na kiungo mfaransa Christopher Nkunku, 24, msimu huu, lakini watasikilia madau yakayovuka au kufikia £63.3m. Manchester United, Liverpool, Paris St-Germain, Real Madrid, Manchester City, Arsenal na Bayern Munich zote zinafuatilia hali ya mambo kwa karibu. (ESPN)
Tottenham imepeleka dau la £2m kwa ajili ya mlinzi wa kati wa Oxford United Luke McNally, 22. (Football Insider)
Liverpool inajiandaa kumsajili winga wa kimataifa wa Scotland Ben Doak,16 kutoka Celtic kwa ada ya £600,000. (Goal)





No comments:
Post a Comment