Fistula: Baada ya kujifungua, fistula ilisababisha harufu mbaya na nilishindwa kuzuia haja'' - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Wednesday, 4 May 2022

Fistula: Baada ya kujifungua, fistula ilisababisha harufu mbaya na nilishindwa kuzuia haja''

 

Sharon Korir

CHANZO CHA PICHA,SHARON KORIR

Maelezo ya picha,

Sharon anaelemisha wanawake nchini keny juu ya athari za fistula

Sharon Korir , ni mama ya watoto wawili kando na hayo yeye ni pia wakili na mwalimu nchini Kenya .

Tukio la mwaka wa 2017 lilisababisha mkondo wa maisha yake kibadilika kabisa , Hii ni baada ya kujifungua mtoto wake wa pili alijikuta katika hali ambayo hakuitarajia .

Kinyume na uzoefu wa kujifungua mtoto wa kwanza na kila kitu kuendelea vizuri baadae anasema kisa cha mtoto wa pili kilikuwa tofauti, alijikuta hawezi kuzuia haja zake kubwa na ndogo .

"Mwaka wa 2017 baada ya tu kujifungua mtoto wangu wa pili , niligundua kwamba nilikuwa na harufu mbaya sana ikitoka kwenye sehemu zangu za siri. Wakati huo sikuwa na habari ni nini kilikuwa kinasababisha uvundo huo'' anasimulia Korir.

Ila anaporudisha akili nyuma anakumbuka mchakato wa kujifungua ambao ulikua na matatizo mengi , Kama kina mama wengi ambao wanabahatika kujifungulia katika hospitali nzuri.

Alielekea katika hospitali mmoja nchini Kenya , anakumbuka akiwa na uchungu wa kawaida unaompata mama kabla ajifungue mtoto , ila uchungu wake ulikithiri kwa muda mrefu kuliko kawaida

Anasema kwamba mchakato mzima wa wahudumu wa afya kuwa walichukua muda huo , pamoja na kwamba mtoto alichoka sana tumboni na ikawa ni vute ni kuvute katika shughuli ya mtoto kuingia ulimwenguni anasema kwamba mambo yalifanyika kwa haraka sana.

"Nilikaa kwa masaa mengi kwa uchungu wa kujifungua kwa hio wakati ulipowadia wa kujifungua , mtoto alitoka kwa nguvu au kishindo na kupelekea kuta za kizazi changu kuraruka kabisa , kuanzia sehemu ya mbele hadi nyuma .na kiliacha shimo kubwa hapo "Korir anakumbuka .

W

CHANZO CHA PICHA,SHARON KORIR

Baada ya kurudi nyumbani aligundua kwamba hakuwa na uwezo wa kushikilia haja zake kubwa wala ndogo.

Aidha Sharon anasema kwamba njia za haja kubwa na ndogo pia zilikuwa kana kwamba zilibadilishana , ikawa haja kubwa inatoka kwa upande wa mbele na haja ndogo upande wa nyuma. Ni matukio ambayo yalimpa mshtuko mkubwa .

"Nilikuwa nimejifungua hapo awali , na sikuwahi kuwa katika hali kama hii, kwa hio nilihisi mabadiliko makubwa , ni vipi haja ndogo imenitoka na sijagundua ? nilijiuliza , ala ni vipi ni na harufu mbaya ambayo sielewi inatokea wapi" anasema Sharon.

Mama huyu anasema kwamba kwa kipindi cha wiki kama sita alikuwa katika hali ya mshtuko mkubwa , ikiandamana na sonona ya hali ya juu asijue la kufanya.

Upande mmoja alikuwa na uoga kutokana na kuona kwamba mwili wake haukuwa unastahimili haja zake , na kila wakati zilitoka bila ya ufahamu wake .Kilichofuata baadaye ni siku nyingi za ukimya na usiri mkubwa .

Safari ya kutafuta Tiba

"Kwa kukosa raha na kukata tamaa, nilianza kutafuta matibabu ya hali yangu na ndipo nilipoambiwa nina Fistula aina ya Recto -Vaginal. Hii ilikuwa imetokea baada ya kujifungua na ilielekea kwamba kule kukawia kwangu kabla ya kujifungua kulisababisha mtoto kuniacha na majeraha mabaya . " anasema Sharon

Sharon anasema licha ya kwamba baada ya mtoto kutoka alishonwa maeneo yaliokuwa yamepasuka , bado makovu mengine yalisalia ndani ya mwili wake .

Hali ilielekea kwamba njia za haja zake zilikuwa zimekaa vibaya na kwa kawaida lazima mwili wa binadamu utatoa haja hizo kwa vyovyote vile yeye alijikuta kwamba hakuwa ana uwezo wa kuzuia kutoka kwake .

"Nilipatwa na kiwewe. Nilikuwa na maswali mengi yasiyo na majibu, Ilinibidi kufanyiwa upasuaji wa kurekebisha hali yangu , ilichukua miezi mingi ya matibabu hadi nilipopona.'' Anaeleza Sharon

w

CHANZO CHA PICHA,SHARON KORIR

Maelezo ya picha,

Sharon anatamani kufungua shirika la kuelemisha kuhusu Fistula

Kuwa mwanaharakati wa fistula

Mwezi huu wa Mei Dunia itakuwa ikiangazia siku ya Fistula duniani na husuan tarehe 23 ndio siku iliyotengwa kwa dunia kuendelea kuhamasishwa na kuzungumzia hali hii.

Sharon anasema kwamba yeye ni mmoja wa wanaharakati ambao wanafahari na siku hii licha ya kuwa ana makovu ya Fistula

Baada ya kupona Sharon Korir aliamua kwamba hataki kuona mwanamke mwengine anapitia alichokipitia baada ya kuuguza Fistula na kupitia hali ngumu ya kupona.

Na kwakuwa yeye ni Wakili na mwalimu mtawalia alielewa kwamba alikuwa na nafasi nzuri ya kuelimisha jamii kupitia simulizi lake , akilenga wanawake ambao wanapitia madhila aliyowahi kuwa nayo.

Je ugonjwa wa Fistula nini ?

Fistula ni ugonjwa ambao husababisha shimo kubwa kati ya njia ya uzazi na njia ya mkojo unatokana na mama kuwa na uchungu wa muda mrefu wakat iwa kujifungua.

Na mtoto anapotoka kwa nguvu anasababisha maumivu makali, iwapo mama atakosa matibabu basi hali hio inatambulika kama Fistula.

Kwa mujibu wa shirika la UNFPA mara nyingi ugonjwa huu huwapata wanawake na wasichana masikini kabisa na wanaotoka jamii zilizotengwa, ambao mara nyingi hujifungulia katika mazingira yaliyo nje ya hospitali au mbali na wataalam wa afya ya uzazi.

Matibabu ya ugonjwa huu ni marekebisho ambayo hufanywa kupitia upasuaji maalum.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here