Mazoezi ya asubuhi ya mapema yanatajwa kuwa ni muhimu na yenye afya kwa wanawake wanaotaka kupunguza uzito na kupunguza hatari ya kupata shinikizo la damu.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa nchini Marekani, mazoezi ya viungo ni mazuri kwa afya yako bila kujali muda wa siku unaofanya, lakini muda wa kufanya mazoezi katika siku husika na kupata matokeo mazuri hutofautiana kati ya wanaume na wanawake.
Uchunguzi unaonyesha kuwa wanawake hupoteza mafuta mengi wakati wa kufanya mazoezi asubuhi, wakati wanaume hupoteza uzito zaidi wakati wa kufanya mazoezi jioni.Hii ni kwa mujibu wa matokeo ya kisayansi yaliyotokana na wanaume na wanawake walioshiriki katika utafiti huo, kwa mujibu wa watafiti waliofanya utafiti huo.
Utofauti wa homoni, nguvu za kimwili na usingizi kwa wanawake na wanaume zinaweza kuwa na mchango mkubwa kwenye hili.Utafiti huo uliohusisha wanaume 30 na wanawake 26 - wote wakiwa timamu na wenye afya njema na umri kati ya miaka 25 na 55 - ulidumu kwa wiki 12 na kufuatilia matokeo ya aina tofauti za mazoezi.

No comments:
Post a Comment