Muda tunaotumia tukiwa macho na kulala ukilinganisha na jamaa zetu wakiwemo nyani huenda ulisaidia sana katika mabadiliko yetu. Katika usiku kavu, wawindaji wa San wa Namibia mara nyingi hulala chini ya nyota. Hawana taa za umeme au matoleo mapya ya filamu za Netflix ili kuwaweka macho.
Hata hivyo wanapoamka asubuhi, hawajalala saa nyingi zaidi ya mkaazi wa kawaida wa jiji la Amerika Kaskazini au Ulaya ambaye amekuwa macho akitazama simu zao. Kulingana na mwanaanthropolojia wa mageuzi David Samson wa Chuo Kikuu cha Toronto huko Mississauga, utafiti umeonyesha kuwa watu katika jamii zisizo za kiviwanda ambazo hukaribia sana na mazingira ambayo spishi zetu ziliibuka - hulala chini ya masaa saba kwa usiku.
Hii inashangaza unapozingatia jamaa zetu wa karibu kwamba mwanadamu hulala saa kidogo kuliko tumbili. Sokwe hulala takribani saa 9.5 kwa siku na nyani wenye vichwa vyeupe hulala kama masaa 13. Samson anaita hitilafu hii kuwa kitendawili cha usingizi wa mwanadamu.
"Inawezekanaje sisi ni nyani ambao hulala muda kidogo?" anauliza.Usingizi unajulikana kuwa muhimu kwa kumbukumbu yetu, kinga ya mwili, na mambo mwngine ya afya yetu.
Mamilioni ya miaka iliyopita, babu zetu waliishi, na labda walilala, kwenye miti. Hata leo, sokwe na nyani wengine hulala kwenye vitanda au maeneo ya muda kwenye miti. Wanapinda au kuvunja matawi ili kuunda umbo la bakuli, ambalo wanaweza kutandika matawi ya majani (nyani kama sokwe pia wakati mwingine hujenga vitanda chini).
Wazee wetu walitoka kwenye miti ili kuishi chini na wakati fulani walianza kulala huko pia. Hii inamaanisha walilazimika kuacha faida zote za kulala kwenye miti, pamoja na usalama kutoka kwa wanyama wanaowinda kama vile simba.
Mabaki ya mababu zetu hayaonyeshi jinsi walivyokuwa wamepumzika. Ili kujua jinsi wanadamu wa kale walivyolala, wanaanthropolojia wametafuta ushahidi bora walio nao: jamii za kisasa zisizo za kiviwanda.
"Ni heshima kubwa na nafasi kubwa kufanya kazi na jumii hizi," anasema Samson, ambaye amefanya kazi na wawindaji wa Hadza nchini Tanzania, pamoja na vikundi mbalimbali nchini Madagascar, Guatemala na kwingineko.
Ili kuweka pamoja historia ya mabadiliko ya usingizi wa mwanadamu, David Samson aliweka kile anachokiita dhana yake ya usingizi wa kijamii ya Anthropolojia ya mwaka 2021.
Kulingana na Samson, usingizi mfupi na wenye kunyumbulika huenda uliibuka kutokana na tishio la uwindaji wakati wanadamu walipoanza kulala chini. Na anadhani sababu nyingine wa kulala salama ardhini ilikuwa ni kulala kwenye kundi.
"Tunapaswa kuzingatia kambi za kwanza za wanadamu na vikundi kama ganda la konokono," anaelezea.
Vikundi vya wanadamu viliweza kushiriki makazi rahisi. Moto uliweza kuweka watu joto na kuzuia wadudu. Baadhi waliweza kulala huku wengine wakisimama kutazama.
Kulingana na Isabella Capellini, mwanaikolojia katika Chuo Kikuu cha Malkia huko Belfast, Ireland Kaskazini, ni jambo linaloweza kukubalika kwamba tishio la wanyama wanaowinda wanyama wengine lilifanya wanadamu wasilale usingizi kidogo kuliko nyani wanaoishi kwenye miti.
Katika utafiti wa 2008, yeye na wenzake waligundua kuwa mamalia walio katika hatari kubwa ya kuwindwa walilala kidogo, kwa wastani.
Lakini Bi Capellini hana uhakika kwamba usingizi wa binadamu ni tofauti na ule wa nyani wengine kama inavyoonekana. Anasema kwamba data iliyopo juu ya usingizi wa nyani inatoka kwa wanyama walio vizuizini.
"Bado hatujui mengi kuhusu jinsi wanyama hulala porini," anasema.
Katika zoo au maabara, wanyama wanaweza kulala chini ya kawaida, kutokana na matatizo. Au wanaweza kulala zaidi, Bi Capellini anasema, "kwa sababu tu wanyama wamechoka". Pia, hali ya kawaida ya maabara - saa 12 mwanga, saa 12 giza - inaweza kutofautiana na kile mnyama hupitia porini mwaka mzima.
Katika utafiti wa 2008, Rattenborg na wenzake walifunga mashine za elektroniki kwenye wanyama watu wa porini na wakagundua kuwa wanyama hao walilala karibu saa 9.5 kwa siku. Utafiti wa awali wa wanyama hao ulirekodi karibu saa 16 za kulala kwa siku.
Kuwa na data kutoka kwa wanyama pori zaidi kungesaidia watafiti wa usingizi.
"Lakini kiufundi ni vigumu kupata," anasema Rattenborg.
Ikiwa wanasayansi wangekuwa na picha wazi ya kulala kwa nyani porini, inaweza kuibuka kuwa usingizi wa mwanadamu sio mfupi sana kama inavyoonekana. Yetish, ambaye anachnguza usingizi katika jamii ndogo ndogo, ameshirikiana na Samson katika utafiti.
Yetish anaelezea jioni ya kawaida kati watu wa Tsimane: baada ya kutumia siku kufanya kazi mbalimbali, kikundi hukusanyika karibu na moto wakati chakula kinapikwa. Wanashiriki chakula, kisha wanakaa karibu na moto gizani.
Watoto na akina mama polepole husogea kwenda kulala, wakati wengine hukaa macho, wakizungumza na kusimulia hadithi.
Hii ndiyo sababu Yetish anapendekeza kwamba wanadamu wa kale walilala ya saa chache kwa kubadlishana habari na utamaduni kando ya moto.
"Ghafla ulifanya saa hizo za giza kuwa na matokeo mengi," asema.
Huenda babu zetu walipunguza usingizi wao kwa muda mfupi kwa sababu walikuwa na mambo muhimu zaidi ya kufanya usiku kuliko kupumzika. Swali la ni kiasi gani tunalala ni tofauti na swali la kiasi gani tungependa kulala.
Samson na wengine waliwauliza washiriki wa somo la Hadza jinsi walivyohisi kuhusu usingizi wao wenyewe. Kati ya watu 37, 35 walisema walilala "ya kutosha", timu hiyo iliripoti hilo mnamo 2017.
Kiwango cha wastani walicholala katika utafiti huu kilikuwa kama saa 6.25 kwa usiku. Lakini waliamka mara kwa mara, wakihitaji zaidi ya saa 9 kitandani kupata hizo saa 6.25 za usingizi. Kinyume chake, uchunguzi wa 2016 wa karibu watu 500 huko Chicago uligundua kuwa walitumia karibu muda wao wote kitandani kulala na walilala kama Hadza.
Bado karibu asilimia 87 ya waliohojiwa katika uchunguzi wa 2020 wa watu wazima wa Amerika walisema kwamba angalau siku moja kwa wiki hawakuhisi kupumzika. Kulingana na Samson, ufahamu bora zaidi wa mabadiliko ya usingizi wa mwanadamu unaweza kuwasaidia watu kupumzika vizuri, au kujisikia vizuri kutokana na mapumziko ambayo tayari wanapata.
"Watu wengi Kaskazini na Magharibi wanapenda kulalamikia na kukosoa usingizi wao," anasema.






No comments:
Post a Comment