Kiungo wa kati wa Leeds United na England Kalvin Phillips, 26, ameiambia klabu hiyo anataka kuondoka msimu huu ili kujiunga na Manchester City. (Football Insider)
City wanaamini kwamba ofa ya takriban £45m-50m itaishawishi Leeds kumuuza, na inafikiriwa Phillips atashinikiza kuhama mara baada ya ofa kuwasilishwa. (Athletic)
Wawakilishi wa kiungo wa kati wa zamani wa Manchester United Paul Pogba wanakaribia kukamilisha mkataba wa miaka minne kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa, 29, kujiunga na Juventus kwa uhamisho wa bure. (Sky Sports)
Juventus wanatarajia Pogba kusaini mkataba nao mwanzoni mwa mwezi ujao baada ya kufikia makubaliano ya maneno. (Guardian)Tottenham, Newcastle na Aston Villa ni miongoni mwa vilabu vya Ligi kuu ya England vinavyomfuatilia mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 32, ambaye ni mchezaji huru baada ya mkataba wake na Real Madrid kumalizika mwishoni mwa msimu huu. (Sun)
Gareth Bale
Chelsea wameanza mazungumzo juu ya kurejea kwa mkopo Romelu Lukaku kwenda Inter Milan, lakini mshambuliaji huyo wa Ubelgiji, 29, atalazimika kukatwa mshahara. (Telegraph)
Inter wana uhakika wa kufikia makubaliano ya kumnunua Lukaku, licha ya tofauti ya kiasi cha £4.3m katika tathmini ya ada ya mkopo ya vilabu. (Sky Sports)
Everton wamekamilisha usajili wa beki wa Uingereza James Tarkowski, 29, kwa uhamisho huru kutoka Burnley lakini mpango huo hautarajiwi kutangazwa hadi mwisho wa Juni. (Liverpool Echo)
Manchester United wanapigiwa upatu kumsajili kiungo wa kati wa Porto na Ureno Vitinha, 24, ambaye ana kipengele cha kuuzwa chenye thamani ya £34m. (Abola)
Matumaini ya Chelsea kumsajili mlinzi wa Sevilla na Ufaransa Jules Kounde hayatakama licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kufanyiwa upasuaji wiki hii. (Standard)
Kounde
Arsenal bado wanaweza kumsajili kiungo wa kati wa Hispania Marco Asensio, 26, msimu huu huku mzozo kuhusu mshahara wake Real Madrid ukiendelea. (Sun)
Asensio, ambaye amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake, angependa kusalia Real Madrid lakini anaamini anastahili nyongeza ya mshahara. (Marca)
Real Madrid wanatumai kumsajili kiungo wa kati wa Borussia Dortmund na Uingereza Jude Bellingham, 18, licha ya ushindani kutoka kwa timu za Ligi kuu England za Manchester United na Liverpool kuhusu mkataba wa £78m. (Metro)
Southampton wamefikia makubaliano na Manchester City kumsajili kipa wa Ireland Gavin Bazunu, 20. (90min).
Bournemouth wanakaribia kumsajili beki wa West Ham Muingereza Ryan Fredericks, lakini Fulham pia wanamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29. (Football Insider)



No comments:
Post a Comment