Tetesi za soka Ulaya Jumapili tarehe 12.06.2022: Lewandowski, Nunez, Mane, Richarlison, Nkunku, Pogba, Leno - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Sunday, 12 June 2022

Tetesi za soka Ulaya Jumapili tarehe 12.06.2022: Lewandowski, Nunez, Mane, Richarlison, Nkunku, Pogba, Leno

 

Marco

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Marco Asensio

Arsenal ni miongoni mwa vilabu vichache vinavyomtaka mshambuliaji wa Real Madrid, raia wa Hipsania, Marco Asensio, ambaye hatma yake itafahamika wiki ijayo.

Tottenham wako kwenye mazungumzo mazuri ya kumsajili mshambuliaji wa Everton na Brazil Richarlison, 25, kwa ada ya £51m. (UOL Esport - in Portuguese)

Chelsea wamepata imani kubwa ya kumsajili winga mfaransa, Ousmane Dembele baada ya klabu yake ya Barcelona kuthibitisha kwamba Dembele, 25, hajasaini mkataba mpya. (Sun)

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Christopher Nkunku, 24, anatarajia kubaki RB Leipzig na kusaini mkataba mpya licha ya kusakwa na Manchester United na Chelsea. (Leipziger Volkszeitung - in German)Manchester United itaingia katika mbio za kumsaka mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski iwapo ndoto za mkongwe huyo mwenye miaka 33 kwenda Barcelona zitashindwa kutimia, wakatii huu wakali hao wa Hispania wakijaribu kwanza kuuza wachezaji wake wanaolipwa mkwanja mrefu. (Sun)

Lewa

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Chelsea pia wanajiandaa kuingia kwenye mbio za kumuwania Lewandowski, lakini hawawezi kupeleka ofa mpaka wamuuze mshambuliaji mbelgiji, 29 na anayeshika rekodi ya usajili ya klabu ya £97.5m, Romelu Lukaku. (Star)

Arsenal ni moja ya klabu kadhaa zinazofuatilia kinachoendelea kwa Marco Asensio pale Real Madrid, hatma ya kiungo huyo mshambuliaji wa Hispania mwenye miaka 26 itajulikana wiki ijayo.

Liverpool imefikia makubaliano ya kumnunua mshambuliaji wa Uruguay, Darwin Nunez, 22 kutoka Benfica na sasa wanaanda mkataba tu kukamilisha uhamisho huo wenye thamani ya £85m. (Guardian)

Nunez

CHANZO CHA PICHA,NUNEZ

Maelezo ya picha,

Nunez

Uhamisho huo wa Nunez unamaanisha kuwa mshambuliaji wa Senegal Sadio Mane, 30, anakaribia kutimka Liverpool kuhamia Bayern Munich. (Telegraph - subscription required)

Kiungo mfaransa Paul Pogba, 29, atarejea Juventus kwa mkataba wa miaka minne wenye thamani ya £68m baada ya kuachana na Manchester United. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Arsenal iko kwenye mchakato wa kumuuza kipa mjerumani Bernd Leno, 30, kwenda Fulham katika uhamisho wa kushangaza. (Sun)

Fulham pia wana matumaini ya kumalizana na nyota wawili wa Liverpool, mlinzi wa pembeni raia wa Wales, Neco Williams, 21 na mshambuliaji mjapani Takumi Minamino, 27. (90min)

Kiungo wa Switzerland Granit Xhaka, 29, anasakwa na Bayer Leverkusen wakati huu ambapo Arsenal anakaribia kumnasa kiungo mchezeshaji wa Ubelgiji Youri Tielemans, 25, kutoka Leicester. (Mirror)

Granit Xhaka

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Granit Xhaka

Liverpool inaangalia uwezekano wa kumruhusu mlinzi muingereza Nat Phillips, 25, kurejea Bournemouth kwa mkopo msimu ujao. (Mirror)

Luis Suarez bado hajaamua hatma yake lakini Aston Villa inataka kumsajili mshambuliaji huyo mruguay mwenye miaka 35. (Mundo Deportivo)

Juventus iko kwenye mazungumzo na Atletico Madrid kumsajili kwa mkataba wa kudumu mshambuliaji wa zamani wa Chelsea mhispania, Alvaro Morata, 29. (TuttoSport - in Italian)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here