Ujasusi wa Uingereza: Urusi yahamishia mifumo ya ulinzi katika kisiwa cha nyoka - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Monday, 6 June 2022

Ujasusi wa Uingereza: Urusi yahamishia mifumo ya ulinzi katika kisiwa cha nyoka

 

Kulingana an ujasusi wa Uingereza, mifumo ya ulinzi ya Urusi inapelekwa katika Zmeinoye
Image caption: Kulingana an ujasusi wa Uingereza, mifumo ya ulinzi ya Urusi inapelekwa katika Zmeinoye katika Kisiwa cha Nyoka

Ujumbe wa ujasusi wa kijeshi wa Uingereza unaoripoti kuhusu hali katika Ukraine unasema kuwa baada ya kupoteza meli ya Moskva, jeshi la Urusi limehamisha mifumo yao ya ulinzi wa mashambulizi ya anga, ikiwemo mifumo ya Tor na Pantsir , na kuipeleka katika Kisiwa cha nyoka kilichopo katika Bahari nyeusi.

"Huenda, silaha hizi zimetengenezwa kwa ajili ya kutoa ulinzi wa mashambulio ya anga kwa meli za kivita za Urusi karibu na kisiwa cha Zmeiny ," Ujasusi wa Uingereza unasema. Kwa maoni yake, hatua za jeshi la Urusi karibu na Zmeinoye "zilisaidia kufunga eneo la mwambao wa Ukraine na kuzuia kuanzishwa tena kwa biashara ya majini, ikiwemo kusafirisha nafaka za Ukraine nje."

Ukraine na nchi za Magharibi wanaishutumu Urusi kwa kuzuia mauzo ya nje ya chakula kutoka katika bandari za Ukraine.

Nchi nyingi duniani hutegemea nafaka kutoka Ukraine, ambapo ukosefu wake unatishia baa kubwa la njaa.

Taarifa ya mkuu wa ujasusi wa Uingereza pia ilisema kuwa Jumapili asubuhi Urusi ilifanya shambulio la kombora kutoka majini la Kh-101 kwenye miundo mbinu ya leri mjini Kyiv katika kile kilichokuwa ‘’jaribio la usambazaji wa silaha za Magharibi kwa jeshi la Ukraine katika maeneo ya vitani."

Kiwanda cha ukarabati wa magari cha  Darnytsia Carriage baada ya shambulio la Urusi
Image caption: Kiwanda cha ukarabati wa magari cha Darnytsia Carriage baada ya shambulio la Urusi

Urusi inadai kwamba shambulio la Jumapili katika Kyiv liliharibu vifaru vilivyotolewa na nchi za Magharibi kwa Ukraine. Lakini kulingana na Kyiv, kiwanda cha ukarabati wa magari ndiokilichoharibiwa kidogo, na kwamba hapakuwa na zana za kijeshi. Maafisa wa Ukraine waliwaalika waandishi wa habari kwenye kiwanda hicho na kuwaonyesha kiwango cha uharibifu uliofanyika.

Kuhusu hali katika jimbo la Donbass, Uingereza imeandika kuwa mapigano makali yanaendelea katika Severodonetsk, na "Vikosi vya Urusi vimeendelea na mashambulizi vikisonga kuelekea Sloviansk, vikijaribu kuzingira vikosi vya Ukraine.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here