MAANDALIZI YA MAONESHO YA NANENANE KITAIFA MBEYA YAFIKIA ASILIMIA 99 - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Thursday, 28 July 2022

MAANDALIZI YA MAONESHO YA NANENANE KITAIFA MBEYA YAFIKIA ASILIMIA 99

 

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Comred Juma Zuberi Homera amesema maandalizi ya maonesho ya nane nane kitaifa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yamekamilika kwa asilimia 99.

Kwa Mujibu wa Homera maonesho hayo yanafanyika katika viwanja vya John Mwakangale kuanzia Agosti Mosi hadi 8/8/2022 ambapo mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa maonesho hayo Agosti Mosi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Philipo Isdory Mpango

Kaulimbiu ya maonesho ya nanenane mwaka huu ni Ajenda 10/30 Kilimo ni biashara ,shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo,Mifugo na Uvuvi.

Kanda ya Nyanda za Juu Kusini inajumuisha mikoa ya Ruvuma,Mbeya.Njombe.Songwe.Rukwa,Katavi na Iringa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here