Mwalimu mkuu wa Nigeria ahukumiwa kifo baada ya mauaji ya mwanafunzi - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Thursday, 28 July 2022

Mwalimu mkuu wa Nigeria ahukumiwa kifo baada ya mauaji ya mwanafunzi

 

th

Mahakama kuu katika mji wa kaskazini mwa Nigeria wa Kano imemhukumu kifo mmiliki wa shule ya msingi na rafiki yake kwa kunyongwa kwa utekaji nyara na mauaji ya mwanafunzi mwenye umri wa miaka mitano.

Abdulmalik Tanko na rafiki yake Hashimu Isiyaku walipatikana na hatia siku ya Alhamisi.

Mwanamke, anayesemekana kuwa mpenzi wa zamani wa Bw Tanko, amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kwa kuhusika katika utekaji nyara huo.

Wafungwa hao walikiri makosa na kuomba wasamehewe wakati wa kutoa hukumu hiyo.

Adhabu za kifo hazifanyiki nchini Nigeria na wale wanaopatikana na hatia huwa wanakaa gerezani kwa muda usiojulikana.

Wanaume hao wawili walimteka nyara msichana huyo mnamo Desemba 2021 na mwili wake ulipatikana Januari mwaka huu.

Kutekwa nyara kwa Hanifa Abubakar kulizua ghadhabu kote nchini Nigeria.

Tanko alikuwa amedai fidia ya $14,600 (£12,000) kutoka kwa wazazi wa mwathiriwa.

Alikamatwa na polisi na kisha akawaongoza wapelelezi hadi mahali ambapo walikuwa wameuzika mwili wa msichana huyo.

Katika miaka ya hivi karibuni, Nigeria imekuwa ikikabiliana na mzozo mkubwa wa utekaji nyara.

Lakini utekaji nyara wa wanafunzi kwa kawaida umekuwa ukifanywa na makundi yenye silaha.

Takriban wanafunzi 1,500 walikuwa wametekwa nyara na magenge tangu Desemba 2020. Wengi wa waathiriwa wameripotiwa kuachiliwa baada ya malipo ya fidia.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here