Wananchi nchini Tanzania wameamka na bei mpya ya mafuta jumatano ikiwa imepanda kutoka bei ya awalibaada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) kutoe bei elekezi kwa mwezi Agosti.
Kwa sasa bei ya rejareja kwa mafuta ya petroli katika jiji la Dar es Salaam itakuwa Shilingi 3,410 kwa lita kutoka shilingi 3,220 ya awali ikiwa ni ongezeko la kiasi cha shilingi 190.
Kwa upande wa dizeli sasa yatauzwa kwa shilingi 3,322 kwa lita ambayo ni ongezeko la shilingi 179 ambapo mwezi uliopita bei elekezi ilikuwa ni shilingi 3,143
Bei elekezi kwa mafuta ya taa ya sasa ni 3,765 kwa lita kutoka shilingi 3,442 ya awali.
Kwa mujibu wa Mamalaka ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), bei hizo zimejumuisha ruzuku ya Sh100 bilioni iliyotolewa na Serikali.
Ewura inabainisha kuwa bila ruzuku bei ya mafuta ingekuwa juu zaidi ambapo kwa lita ya petroli ngeuzwa 3,630 na dizeli ingekuwa shilingi 3,734 kwa Dar es Salaam.
‘Bei za mafuta katika soko la dunia zinaendelea kupanda na hivyo kusababisha bei ya mafuta katika soko la ndani pia kuongezeka. Ili kupunguza athari za ongezeko hilo kwa wenyeji, Serikali imetoa ruzuku ya TZS 100 bilioni kwa ajili ya mafuta ya Agosti 2022’, ilieleza taarifa waliyoitoa
Kupanda huko kwa bei kumezua maoni mseto na mijadala katika mtandaoni:

No comments:
Post a Comment