'Kila kitu kina mwisho wake' - Je hatma ya Ronaldo ni ipi Man United? - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Tuesday, 25 October 2022

'Kila kitu kina mwisho wake' - Je hatma ya Ronaldo ni ipi Man United?

 

.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Cristiano Ronaldo

Cristiano Ronaldo huenda hakucheza wakati Manchester United ilipookoa pointi mója muhimu dhidi ya Chelsea Jumamosi, lakini bado aliishia kuwa moja ya pointi kuu za mazungumzo.

Kukataa kwa mshambuliaji  huyo kuingia kama mchezaji wa akiba katika ushindi wa 2-0 Jumatano dhidi ya Tottenham, na uamuzi uliofuata wa kuondoka Old Trafford kabla ya filimbi ya mwisho, kumetawala vichwa vya habari katika wiki moja ambayo United inapaswa kusherehekea kupata pointi nne muhimu kutoka kwa nne bora dhidi ya wapinzani.

Wachezaji wakishangilia bao la dakika za lala salama la Casemiro kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, Ronaldo hakujulikana aliko baada ya kuondolewa kwenye kikosi kama adhabu ya meneja wa United Erik ten Hag.

Mholanzi huyo alisisitiza kuwa kikosi chake bado "kinamhitaji" Mreno huyo lakini maswali yanasalia kama kurejea kwake katika uwanjani kutatuliwa kwa njia isiyo ya kawaida.Nahodha wa zamani wa Manchester United Gary Neville anaamini kuwa sasa ni suala la lini tu, sio ikiwa, Ronaldo ataondoka msimu huu.

"Cristiano Ronaldo atalazimika kwenda mahali pengine na kucheza kila wiki kwa sababu hawezi kukubali kuwa kwenye benchi," alisema kwenye Sky Sports. "Hiyo ni sawa, lakini malizia wiki hii au jenga suluhu ya kufika Kombe la Dunia na kisha umalize.

 'Lazima iishe'

Je hakuna njia ya kurudi ?

Kitendo cha Ronaldo katika dakika chache za mwisho dhidi ya Spurs kimezua mjadala mkubwa, lakini kuna hisia kubwa kuwa hakuna mapatano .

Kocha wa Manchester United Erik ten Hag alionyesha uwezo wake kwa kumtoa Ronaldo kwenye mechi ya Chelsea na kumtenga kufanya mazoezi na kikosi chake cha kwanza.

Matukio ya shangwe miongoni mwa wachezaji wa Manchester United baada ya Casemiro kusawazisha dakika ya 94 dhidi ya Chelsea yalisisitiza kile ambacho Ten Hag anajaribu kulinda huku wakionyesha mapambano, ari na umoja.

"Nina shaka iwapo Ronaldo atachezea Manchester United tena," mlinda mlango wa zamani wa Uingereza Rob Green alisema kwenye BBC Radio 5 Live.

"Ni talaka mbaya lakini Ten Hag amesubiri kwa muda. Ronaldo ameharibu kila kitu ."

Wiki chache zilizopita Ronaldo alisifiwa kwa kufikisha mabao 700 katika historia ya soka. Akiwa na umri wa miaka 37, muda hauko upande wake tena na watu wengine wanaweza kuelewa maonyesho yake ya kuchanganyikiwa huku akitafuta sana wakati wa mchezo.

Beki wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdinand anaamini kuwa hali hiyo ingetatuliwa vyema.

"Singekuwa na furaha kama mchezaji lakini hisia wakati mwingine hukuondolea ubinadamu ," alisema.

"Labda mawasiliano hayajawa wazi wakati wa kushughulika na Ronaldo -  mchezaji bora zaidi kuwahi kucheza, pamoja na Lionel Messi.

 "Anahitaji mawasiliano hayo sasa kuliko wakati mwingine wowote. Yeye ni Rafiki yangu na unataka kuona marafiki zako wakifanya vizuri lakini singeunga mkono hilo kwenye chumba cha kubadilishia nguo. Ikiwa mawasiliano hayapo, matatizo hutokea."

Kiungo wa zamani wa Manchester United Roy Keane aliongeza: "Wachezaji wamefanya vibaya sana Manchester United.

 "Je, kuna njia ya kurudi kwake? Sina hakika."

Ruka Twitter ujumbe
Maelezo ya video,Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa Twitter ujumbe

Ten hag hajafunga mlango

Lakini licha ya kile mbacho wachunguzi wanafikiria, Ten Hag hajafunga mlango kwa Ronaldo.

Alikuwa mfungaji bora wa Manchester United msimu uliopita na aliokoa timu yake mara nyingi kwa mabao ya dakika za lala salama.

Alipoulizwa ikiwa timu ilimkosa Ronaldo Jumamosi, Ten Hag alisema: "Daima.

"Anaweza kufunga mabao na ni wa thamani kwetu. Tunamuhitaji, hilo liko wazi. Nadhani nimesema vya kutosha kuhusu hali hii."

Ronaldo ana kandarasi na Manchester United hadi msimu ujao wa joto lakini amekuwa akihusishwa na kuondoka katika klabu hiyo kabla ya kandarasi yake kukamilikaa.

Miamba ya Ufaransa Paris St-Germain imependekezwa kama mahali mbapo huenda Ronaldo akakimbilia , ingawa imedaiwa kuwa inaonekana haiwezekani.

Kuhamia Ligi Kuu ya Soka nchini Marekani kumeonekana kuwa chaguo jingine linalowezekana, huku kurejea katika klabu ya zamani ya Sporting Lisbon pia kumesemekana kuwa kumepingwa.

'Lengo lazima liwe kwenye mkakati wa kutoka' - uchanganuzi

Simon Stone wa BBC Sport:

Ronaldo amefanya mambo yote sahihi tangu alipoondoka Old Trafford baada ya kukataa kuingia dakika za mwisho dhidi ya Tottenham wiki iliyopita.

Lakini suala la msingi linabaki.

.
Maelezo ya picha,

Cristiano Ronaldo amecheza mechi nane za Premier League msimu huu, huku sita kati ya hizo akitokea benchi

Akiwa na miaka 37, Ronaldo anataka kucheza. Anahisi bado ana uwezo wa kufanya kazi kwa kiwango cha juu na anaweza kutoa mchango wa maana kwenye mechi kubwa.

Kwa upande mwingine, Erik ten Hag anajaribu kuunda timu ambayo inaweza kutawala mpira na kwenda mbele kusaka bao kwa mtindo wa kisasa.

Lakini ni sehemu mbili za msumeno ambazo haziingiliani

Ronaldo anahisi kulikuwa na ofa za kuondoka katika majira ya joto, iwapo angetaka kufanya hivyo . United wanasema hakukuwa na, ofa zaidi ya moja kutoka Saudi Arabia, au angalau hakuna ambaye hangewahusisha kuendelea kulipa asilimia kubwa ya mshahara wake.

United sasa ina mechi sita za kucheza kabla ya Kombe la Dunia. Ronaldo anahitaji muda wa mchezo. Kwa kuzingatia matukio ya wiki hii, inafaa kila mkufunzi kumtumia mchezaji anayelipwa zaidi kwenye kikosi chake.

Lakini lengo sasa linapaswa kuwa mkakati wa kuondoka.

Kulikuwa na watu huko United wakati wa kiangazi ambao walihisi chumba cha kubadilishia nguo kingekuwa bora bila Ronaldo. Matukio ya wiki hii yanaonyesha ushahidi wa hilo.

Pia ni kweli kwamba,  katika kutoa mpira katika maeneo sahihi kwa mshambuliaji, Ronaldo anaweza kuwa mchezaji mzuri sana wa kushambulia.

Zaidi ya wiki tatu zijazo, ni bora kwa pande zote mbili kuona iwapo wanaweza kufanikiwa bila ya mmoja wao, hata iwapo hiyo inamaanisha United kulipa sehemu ya mshahara wa Ronaldo, au mchezaji kuondoka bila sehemu ya kile anachodai.

No comments:

Post a Comment