Kwanini bei ya Unga wa mahindi inaendelea kuzua gumzo Kenya - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Thursday, 27 October 2022

Kwanini bei ya Unga wa mahindi inaendelea kuzua gumzo Kenya

 

.

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Maelezo ya picha,

Ugali

Kwa kipindi cha miaka minne iliyopita, taifa la Kenya na eneo la Upembe wa Afrika kwa ujumla limepata kiasi kidogo cha mvua na kusababisha ukame, mavuno duni na kuharibika kwa mazao katika baadhi ya maeneo ya nchi hizo.

Hali hii imechangiwa na majanga mengine yaliyotangulia, pamoja na uvamizi wa nzige wa jangwani mnamo 2019, athari za janga la Covid-19 mnamo 2020 na 2021, na usumbufu katika usambazaji wa chakula na pembejeo za kilimo, kufuatia vita vya Ukraine na Urusi. .Ni kwasababu ya matatizo hayo ndiposa serikali iliyopita iliamua kuweka ruzuku katika bidhaa mbalimbali ikiwemo mafuta na Unga wa mahindi ili kumzuia mwananchi wa kipato cha chini kuathirika zaidi.

Vilevile suala hilo lilitumika kama kichocheo katika kampeni za uchaguzi uliopita ili kujaribu kuwavutia wananchi huku kila Mwanasiasa akijaribu kutumia tatizo hilo kuwarai wapiga kura kuwachagua.

Wengi akiwemo rais wa sasa William Ruto walisikika katika majukwaa ya kisiasa wakisema kwamba wangetibu tatizo la bei ya unga punde tu watakapochukua mamlaka.

Hatahivyo wiki kadhaa baada ya serikali mpya kuchaguliwa tatizo hilo limekuwa donda sugu, huku Wakenya wakiendelea kulipa zaidi ya shilingi 200 kwa pakiti ya kilo mbili ya bidhaa hiyo muhimu.

Kwanini Unga wa mahindi ni muhimu

.
Maelezo ya picha,

Bei ya Unga wa mahindi wakati wa serikiali ya rais Mwai Kibaki

Ugali, ni chakula  maarufu nchini Kenya kinachopikwa kwa kutumia unga wa mahindi

Bei ya unga wa mahindi imekuwa ikipanda kwa kasi huku serikali ikihusisha hali hiyo na uhaba wa mahindi nchini Kenya.

Wanauchumi wanakadiria kuwa wakazi wa Kenya wanahitaji angalau magunia milioni 49 ya mahindi kila mwaka ili kutosheleza mahitaji ya ugali nchini, lakini ni magunia milioni 35 pekee nchini yalipatikana kabla ya dirisha la uagizaji bidhaa kufunguliwa Julai 1.

Mtangulizi wa Rais Ruto, Uhuru Kenyatta mnamo, Julai 20, alisema kupanda kwa bei kunatokana na uzalishaji uliokandamizwa na hali mbaya ya hewa, kupanda kwa gharama ya uzalishaji na kupanda kwa bei ya vyakula kote ulimwenguni.

Uhaba wa mahindi nchini Kenya ulisababisha ongezeko kubwa la bei ya unga wa mahindi - kutoka wastani wa kSh120 kwa pakiti ya kilo 2 ya unga wa mahindi hadi kSh230.

  Je serikali mpya  imechukua hatua gani?

.

CHANZO CHA PICHA,IKULU YA RAIS KENYA

Maelezo ya picha,

Rais William Ruto

Muda tu baada ya kuchaguliwa kwa serikali rais William Ruto Wakenya wengi hususan wale wa kipato cha chini walikuwa na matumaini sihaba kwamba , kiongozi mpya  wa taifa angelitatua tatizo hilo kwa haraka iwezekanavyo .

Hii ni kutokana na wito wake wakati wa kampeni kwamba alipania kutatua matatizo yanayowakumba akina mama mboga, waendeshaji wa bodaboda na wale wasio na kazi kupitia kubuni ajira. Wito huu ulimfanya kiongozi huyo kuonekana kama mwokozi wa wanyonge.

Hatahivyo muda tu alipochukua mamlaka rais William Ruto aliondoa ruzuku katika Unga wa mahindi pamoja na mafuta, akidai kwamba ruzuku hizo zilikuwa hazimfaidi raia wa chini na kwamba badala yake zilikiuwa zikiwafaidi watu wachache serikalini.

"Kulikuwa na jaribio la kufadhili unga wa mahindi wakati wa maandalizi ya uchaguzi, mpango ambao ulipata dola milioni 58 kwa mwezi mmoja, bila athari yoyote. Mbali na kuwa ghali sana, uingiliaji kati wa ruzuku ya utumiaji huwa na matumizi mabaya, hupotosha soko na kuleta hali ya sintofahamu, ,” Ruto alinukuliwa akisema.

Hatua hiyo ilipongezwa na wengi waliodhani kwamba ingekuwa suluhu ya tatizo la kupanda kwa bei ya Unga na kwa zaidi mafuta. Kwa kuondoa ruzuku ya mahindi, William Ruto alidhania kwamba bei ya bidhaa hiyo hatimaye ingedhibitiwa na soko la bidhaa nchini Kenya na kushuka bila usaidizi wowote kutoka kwa serikali

Lakini wiki kadhaa baada ya uamuzi huo pakiti ya kilo mbili ya  Unga imeendelea kuuzwa kwa zaidi ya shilingi 200 , huku tatizo hilo ambalo Wakenya walidhani limepata mtatuzi likiendelea kuwa kitendawili kisichoteguka.

No comments:

Post a Comment