Manchester City wameziambia klabu kadhaa - ikiwa ni pamoja na Bayern Munich na Inter Milan - ambazo zimeulizia kuhusu upatikanaji wa mlinzi wa Uholanzi Nathan Ake kwamba haitamuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 mwezi Januari. (90Min)
AC Milan wanajiandaa kuanzisha mazungumzo ya mkataba mpya na mshambuliaji wa Ureno Rafael Leao na wangependa kufikia muafaka kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia.
Chelsea wamekuwa wakihusishwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 na wanafuatilia mazungumzo hayo kwa karibu. (La Gazzetta dello Sport)
AC Milan wanavutiwa na kiungo wa kati wa Chelsea na England Ruben Loftus-Cheek, 26, ambaye mkataba wake na The Blues unafikia kikomo mwaka 2024. (Calciomercato).

No comments:
Post a Comment