Napoli wamekuwa wakihusishwa na mshambuliaji wa Manchester United Cristiano Ronaldo, 37, lakini mkurugenzi wa klabu hiyo ya Italia Cristiano Giuntoli amefutilia mbali iwezekano wa kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno. (DAZN, via Talksport)
Liverpool ndio klabu ya hivi karibuni zaidi kuhusishwa na kiungo wa kati wa Brazil Bruno Guimaraes lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Chelsea na Real Madrid wanaomtaka pia, kama Newcastle United watashindwa kumshawishi mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kusaini mkataba mpya kusalia klabuni hapo. (TNT Sports)
Chelsea inamfuatilia mlinzi wa Inter Milan na Uholanzi Denzel Dumfries, 26, wakati wakijaribu kuongeza upana zaidi kwenye nafasi yao ya beki wa kulia ambayo imepwaya baada ya kuumia kwa mchezaji wa kimataifa wa England Reece James, 22. (90 Min).
Rais wa Inter Milan Steven Zhang anasema mlinzi wa Slovakia Milan Skriniar, ambaye inaaminika anasakwa na Paris St-Germain, hauzwi na "ana imani" mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 atasalia katika klabu hiyo ya Serie A. (Sky Sport Italia, via Football Italia)
Skriniar
Tottenham inaweza kuwaruhusu winga wa Uhispania Bryan Gil, 21, na mlinzi wa Uingereza Japhet Tanganga, 23, kuondoka mwezi Januari, huku pia wakimtoa kwa mkopo beki wa kulia wa Uingereza Djed Spence, 22. (Times)
Juventus wanataka kumpa winga Mwingereza Samuel Iling-Junior, 19, mkataba mpya, huku mazungumzo kati ya pande hizo mbili yakiwa yameanza muda mfupi uliopita. (Calciomercato)
Arsenal wamefanya mazungumzo ya awali kuhusu mkataba mpya na mkurugenzi wa ufundi Edu ambaye amekuwa akihusishwa na majukumu kama hayo barani Ulaya. (Evening Standard)
Edu
Everton wanavutiwa na mshambuliaji wa Ureno Daniel Podence, 27, ambaye mkataba wake na Wolves utaendelea hadi msimu wa joto wa 2024. (Football Insider)
Nottingham Forest inapanga kutumia kati ya £50m na £100m katika dirisha la uhamisho la Januari kusaidia nafasi yao ya kusalia kwenye Premier League. (Football Insider)
Barcelona wanatarajia kusajili mbadala wa kiungo wa kati wa Uhispania Sergio Busquets mwenye umri wa miaka 34 mwezi Januari. (ESPN)
Manchester City wamemsajili kiungo wa kati Emilio Lawrence mwenye umri wa miaka 17 kutoka Everton. (Fabrizio Romano)



No comments:
Post a Comment