Kanisa Halisi la Mungu Baba wanazo Siku Kuu tatu (3) muhimu ambazo ni Sikuu ya Mwaka wa kuanza ambayo ni kila 1 Kiselu, 1Mjira Halisi, Siku Kuu ya Badiliko ambayo ni kila 21Ethanimu na Majira Halisi, na Siku Kuu ya Hija ya Chanzo Halisi ambayo kuiadhimisha kila 26 Thebeti, 1Majira Halisi.
Tarehe za kuadhimisha sikukuu hizi zinatambuliwa na Kanisa Halisi kulingana na tarehe zake ambazo limebaini kuwa ndizo Majira Halisi, tofauti na Kalenda zingine hasa ile ya Gregory ambayo inategemea mwaka husika wa huyo Gregory ukoje.
Kwa mujibu wa Kanisa Halisi, Mwaka 1582, kwa Kalenda ya huyo Gregory, kuna makusudi mabaya yalitokea ya kubadilisha majira iliyokuwepo kabla ya uharibifukama vile; badala ya mwezi kuwa na malango (siku) 28 peke yake ikizingatiwa kuwa mwezi una wiki 4x7= 28); mwezi ukawa na siku 29, 30, 31!
Kanisa Halisi linabainisha kuwa tatizo lililotokea, baada ya kuongezwa siku tatu kwa mwezi, badala ya mwaka kuwa na siku 336 ukawa na siku 365! Hivyo, lile kusudi la tangu Chanzo Halisi la kuwa majira imara na yenye uhalisia ya kumcha Chanzo Halisi (Mungu Baba) kwa mujibu wa (Isa.33:6), likavurugwa.
Tatizo lingine ambalo Kanisa Halisi linabaini kuwa lilijitokeza ni mwaka kuwa na miezi 13 badala ya miezi 12 iliyoandikwa katika kitabu cha Esta 3:7. Hivyo, mtu akiwa na miaka 12, sasa akawa anakuwa na miaka 13! akiwa na miaka 24 akawa anakuwa na miaka 26! akiwa na miaka 35 akawa anakuwa na miaka 39 na akiwa na miaka 60 akawa kumbe anakuwa ana miaka 65!
Kanisa Halisi likabaini kuwa kumbe miaka ya ziada ndiyo iliyokuwa inatunza madhila mabaya kama magonjwa, madhaifu na uzee na kwamba watu washapokea majira kabla ya uharibifu kwa mujibu wa 2 Sam.7:10-11, hakuna kuangamia tena na Kanisa hilo linasisitiza kwamba hilo ni badiliko ambalo limeanzia Tanzania kwenda katika mataifa mengine yote hivyo ni kweli halisi.
Sasa kufuatana na Kalenda hiyo inayoaminiwa na kufuatwa na Kanisa Halisi jana 21 Ehanimu 1 Majira Halisi (Jumapili, Novemba 6, 2022) Kanisa Halisi liliadhimisha kwa mara ya kwanza Sherehe ya Badiliko ambayo kama nilivyoeleza hapo awali sherehe hiyo ni miongoni mwa Sherehe kubwa tatu za Kanisa hilo.
Sherehe hiyo, iliungurumishwa na kutimua vumbi nje ya ukumbi, katika Viwanja vya Makao Makuu ya Kanisa hilo, eneo la Tegeta Namanga mjini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mamia ya Uzao na Wasimamia Sauti kutoka Vituo vya Kanisa hilo vilivyoko katika mikoa mbalimbali Tanzania Bara, Zanzibar na Mataifa ya Nje.
Hakika sherehe hiyo ilikuwa ya kipekee kwa kuwa mbali na kuhudhuriwa na Uzao na wasimamizi wa sauti, lakini pia ilihudhuriwa na Waalikwa mbalimbali wasiokuwa wafuasi ambao walionesha kuwa wenye furaha wakati wote tangu mwanzo hadi mwisho wa Sherehe hiyo.
Licha ya jua kali lililokuwepo, lakini katika Sherehe hiyo iliongozwa na Kiongozi Mkuu wa Kanaisa hilo, watu wote walionekana kufurahi na kutimua vumbi kiwanjani kwa kucheza muziki uliokuwa ukipigwa na bendi ya Kanisa hilo la nyimbo za kumuinua Chanzo Halisi ambapo tangu saa 2 aubuhi hadi saa sita mchana ilipomalizika sherehe hiyo hakuna aliyeonyesha kuchoka.
Baba Halisi alisema Badiliko hilo maana yake ni kwamba sasa Watu wametoka katika Roho na Nafsi vilivokuwa na mambo yote mabaya yaani mauti na sasa wameingia limbuko la Moyo hawako tena katika kuokoka bali wamekobolewa, akisema "Ibada ni Uzalishaji siyo kulialia tena."
"Tunaposema hakuna mauti tena, muelewe kwamba mauti siyo ufukiwe katika udongo, hapana maana yake hapa ni kwamba kifo ni yale yote ambayo kila ukifanya yanaharibika ndiyo mauti, kwa hiyo sasa kwa badikilo hili mauti haya hayapo tena, kila atakayefanya jambo kwa haki litafanikiwa", Baba Halisi akafafanua
Baba Halisi alihitimisha kwa kuongoza Toba ya Hiari ya Moyo kwa Chanzo Halisi (Mungu Baba) kufuta mizozo na vita katika nchi na mataifa mbalimbali duniani.
"Kwa kuwa hatujui kwa nini wana mizozo na vita, tufanye toba ya hiari ya moyo kwa Chanzo Halisi ili kuvuta mizozo na vita hivi, limeshakuwako Badiliko hatutaki vita.", akasema Baba Halisi kisha akaendesha toba hiyo huku Wasimamia sauti wa Vituo vya Kanisa Halisi kutoka nchi za nje waliofika kwenye sherehe hiyo wakiwa wamejipanga mbele yake.
Tafadhali tazama picha za mtiririko wa matukio ya Sherehe hiyo ya Badiliko, hapo👇
Uzao wakishangilia wakati wa Sherehe hiyo ya Badiliko.
Uzao wakiwa wametulia kumsikiliza Baba Halisi wakati akiongoza Sherehe hiyo ya Badiliko.
Uzao wakiwa wametulia kumsikiliza Baba Halisi wakati akiongoza Sherehe hiyo ya Badiliko.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa wametulia kumsikiliza Baba Halisi wakati akiongoza Sherehe hiyo ya Badiliko.
Uzao akiwa katika malezi, huku akiendelea kumsikiliza Baba Halisi wakati akiongoza Sherehe hizyo ya Badiliko.
Baada ya Baba Halisi kufungua Sherehe hiyo kwa kueleza nini maana ya Badiliko, akasema, "sasa bendi pigeni wimbo wa 'mwendokasi' tuchangamke, bendi ikaungurumisha muziki ambao uisababisha uzao kucheza bila kuchoka licha ya jua kali lililokuwepo, maana sherehe hiyo ilifanyika nje kwenye Viwanja vya Kanisa Halisi.👇
Baada ya Sherehe hiyo ya Badiliko kuchangamka, Baba Haisi akaendelea kuiongoza👇
Msimamia Sauti Moja akisoma maandiko kama alivyokuwa ameeekezwa na Baba Halisi wakati akieleza kwamba Badiliko lina maana pia kwamba sasa kila anayetenda kwa hali ameondoka kutoka 'kao la Mauti' akifafanua kwamba mauti haimaanaishi kwamba ni mtu kufukiwa bali ni kuharibikiwa na kila jambo jema analofanya, na kwamba sasa hiyo imekwisha.
Uzao wakipokea shukurani ya kutoka Kao la Mauti ilipokuwa ikiendeshwa na Baba Halisi kwenye Sherehe hiyo ya Badiliko.
Uzao na Waalikwa wakipokea shukurani ya kutoka Kao la Mauti ilipokuwa ikiendeshwa na Baba Halisi kwenye Sherehe hiyo ya Badiliko.
Baadhi ya Uzao wakitoa Matunda (Sadaka) ya Shukurani ya kutoka kao la Mauti.
Baba Halisi akiendesha Shukurani ya Badiliko kutoka Kao la Mauti.
Msimamia Sauti Moja na wenzake wakipokea shukurani hiyo.
Uzao wakishangilia baada ya Baba Halisi kusema "Imekuwaa", kuhitimisha Shukurani ya Badiliko aliyokuwa akiifanya.
Baada ya kufanya shukrani hiyo Baba Halisi akasema, "Sasa wote kwa sauti kubwa; "Sikuzaliwa nife baliniishi niwe baraka kwa wengine" uzao wote wakasema hivyo mara tatu, kisha akaamuru upigwe wimbo uwa Utawala wa Amani.
Wimbo huo ukapigwa na kuamsha heka heka uwanjani👇
Mwiaimbaji wa bendi ya nyimbo za kumuinua Chanzo Halisi akiongza wenzake kuimbwa wimbo huo wa Utawala wa Amani.
Mpulizaji mahiri wa domo la Bata Mwanamuziki nguli King Maluu, akiungurumisha ala hiyo wakati bendi hiyo ya nyimbo za kumuinua Chanzo Halisi wakiimba wimbo huo wa Utawala wa Amani.
Uzao wakiselebuka kila mmoja kivyake kucheza wimbo huo wa Utawala wa Amani 👇
Hadi Uzao wakajaa mbele ya jukwaa la wanamuziki
Mama Halisi akionyesha furaha ya kutosha wakati aliselebuka kucheza wimbo huo wa Utawala wa Amani.
Mama Halisi akiendelea kuonyesha furaha ya kutosha wakati aliselebuka kucheza wimbo huo wa Utawala wa Amani.
Msimaia Sauti Faida na yeye akiselebuka vya kutosha, kucheza wimbo hio wa Utawala wa Amani.
Baba Halisi akiwaangalia Uzao wakati wakiselebuka kucheza wimbo huo wa Utawala wa Amani, wao na yeye wote wakiwa kwenye jua kali la saa sita mchana wakati wa sherehe hiyo ya Badiliko.
Hatimaye naye Baba Halisi akawaunga mkono Uzao kuselebuka Wimbo huo wa Utawala wa Amani.
Baba Halisi akaendelea kuwaunga mkono Uzao kuselebuka Wimbo huo wa Utawala wa Amani.Baba Haisi akiendelea kuselebuka wimbo huo wa Utawala wa Amani.
Hekaheka ya kuselebuka wimbo huo ikiendelea kwa uzao wa rika zote.
Hekaheka ya kuselebuka wimbo huo ikiendelea kwa uzao wa rika zote.Hekaheka ya kuselebuka wimbo huo ikiendelea kwa uzao wa rika zote.
Hekaheka ya kuselebuka wimbo huo ikiendelea kwa uzao wa rika zote.
Hekaheka ya kuselebuka wimbo huo ikiendelea kwa uzao wa rika zote.
Wengine wakabeba hadi viti wakati wakiselebuka kwa furaha kucheza wimbo huo.
Wanamuziki wakimalzia kuimba wimbo huo wa Utawala wa Amani.
KISHA BABA HALISI AKAONGOZA TOBA YA HIARI YA MOYO KULETA AMANI NA KUFUTA VITA KATIKA MATAIFA MBALIMBALI DUNIANI 👇
Baba Halisi akiwata Wasimamia Sauti wa Kanisa Halisi kutoka Mataufa ya Nje kwa ajili ya kufanya Tofa hiyo ya hiari ya Moyo kwa ajli ya kuleta Amani na kufuta Vita katika Mataifa mbalimbali .
"Kwa kuwa hatujui kwa nini hayo mataifa wanapigana vita, basi tufanye Tofa ya hiari ya Moyo kumwendea Chanzo Halisi ili fute magomvi na vita katika mataifa hayo", akasema Bada Halisi baada ya Wasimamia Sauti wa Kanisa Halisi katika Mataifa ya Nje waliokuwa kwenye Sherehe hiyo ya Badiliko, kufika mbele yake.
"Sasa Toba hii ya Hiari ya Moyo tunaifanya kama ile tuliyofanya Mwanza, ninyi nisubirini hapo", akasema Baba Halisi kisha akaondoka akinyuziza Damu Safi (maji) kuzunguka eneo lote la Sherehe hiyo....
Baba Halisi akinyunyiza Damu Safi (maji) huku na huko.
Baba Halisi akiendelea kunyunyiza Damu Safi (maji) huku na huko.
Baba Halisi akiendelea kunyunyiza Damu Safi (maji) huku na huko.
Baba Halisi akiendelea kunyunyiza Damu Safi (maji) huku na huko, huku wasaidizi wake wakiwa sanjari na yeye..
Uzao wakishangilia wakati Baba Halisi akipita kunyunyizaDamu hiyo Safi (Maji).
"Unajua kuna vitu vingine ukifanya, Wanasayansi wanashangaa... hapa nakuwa kama punguwani hivi, lakini imeshakuwa", akasema Baba Halisi kuwaambia Wasimamia Sauti, baada ya kurejea kunyunyiza maji ikiwa ni sehemu ya Toba hiyo ya Hiari ya Moto kufuta mzozo na vita katika mataifa mbalimbali.
Kisha Baba Halisi akaita baadhi ya Wageni walioalikwa katika Sherehe hiyo kuja kusalimia👇
"Unaona hata wenzangu wale palee, nimekuja nao" akasema Mosses wakati akiendelea akaendelea kusalimia Uzao
Uzao wakisikiliza salam za wageni Waalikwa.
"Mimi naitwa Bashir, siyo wa Kanisa hili, lakini kwa ajinsi lilivyo napenda kufanyakazi nalo, leo Jumapili nilikuwa niwe nimepumzika nyumbani, lakini nilipoambiwa na Mkuu wangu wa Kituo nije hapa, nikafurahi nikaja kama mnavyoniona. Asante Baba na Mama Halisi na Uzao wote wa Kanisa hili", akasema Afande huyu.
"Heri Heriii", Baba Halisi akatoa salam kwa Uzao na Waalikwa wote kisha akatangaza tamati ya Sherehe hiyo ya Badiliko, akisema, Sasa baada ya wote kupokea badiliko hili tambueni sasa Ibada ni uzalishaji hakuna kulialia tena kwenye nyumba za Ibada, kila mtu na kila kitu sasa imekuwa badiliko".
Lakini kabla ya kuondoka, akaona dalili za mvua, akasema "mnaona dalili hiyo, mvua karibu itanyesha hebu tufanye shukurani kwa Chanzo Halisi kabla sijaondoka hapa, ili mvua ikinyesha ije ya baraka.
Baba Halisi akafanya shukurani ya mvua hiyo.
Baba Halisi akiondoka baada ya kuhitimisha Sherehe hiyo ya Badiliko.
Baba Halisi naye akiondoka pia mahali hapo.
Uzao akiondoka na watoto wake.Uzao huyu naye akiondoka.
Huduma za Kibenki pia zilikuwepo kutekeleza kaulimbiu ya 'Ibada ni Uzalishaji'
Vijana wakitoa huduma ya kuuza maji ya One Up, kutekeleza kaulimbiu ya 'Ibada ni Uzalishaji'
Mama na Baba Lishe pia walikuwepo kutekeleza kaulimbiu ya 'Ibada ni Uzalishaji'
No comments:
Post a Comment