KONGAMANO LA KIMATAIFA LA SAUTI YA WANASAYANSI ZA JAMII KUFANYIKA NOVEMBA 10-11,2022 UDSM - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Monday, 7 November 2022

KONGAMANO LA KIMATAIFA LA SAUTI YA WANASAYANSI ZA JAMII KUFANYIKA NOVEMBA 10-11,2022 UDSM

  

*********

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Ndaki ya Sayansi za Jamii wameandaa Kongamano la Kimataifa linalohusu Sauti ya Wanasayansi za Jamii ambalo litafanyika Novemba 10 hadi 11, 2022 katika Kampasi ya Mwalimu Nyerere, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Novemba 7,2022 Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti Kamati ya Maandalizi Dkt.Muhidin Shangwe amesema kongamano la mwaka huu linaleta wataalamu wa sayansi za Jamii wapatao 200 kutoka ndani na nje ya Bara la Afrika ili kujadili mienendo ya mabadiliko yanayojitokeza barani Afrika na kwingineko kwenye nchi za Kusini mwa Dunia.

“Kongamano la 7 la Sauti ya Sayansi ya Jamii (VSS2022) linakusudia kupaza sauti za wanataaluma wa Sayansi za Jamii kuhusu mabadiliko yanayoendelea kutokea Duniani na athari zake hususan Kusini mwa Dunia”. Amesema

Amesema katika Kongamano hilo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-UTAFITI, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof.Bernadeta Killian.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here