MKE WA RAIS WA ZANZIBAR AKABIDHI VIFAA VYA KILIMO CHA MWANI - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Monday, 7 November 2022

MKE WA RAIS WA ZANZIBAR AKABIDHI VIFAA VYA KILIMO CHA MWANI

 


Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi pia Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation “ZMBF” (kushoto) alipokuwa  akisalimiana na Viongozi mara alipowasili kijiji cha   Bweleo  jimbo la Dimani Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi  wakati alipofanya ziara ya kukabidhi vifaa mbali mbali ya Kilimo cha zao la Mwani leo kwa kikundi cha “Ukweli ni Njia  Safi Bweleo” .  .[Picha na Ikulu] 07/11/2022. 

 Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi pia Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation “ZMBF” (katikati) alipokuwa  akitoa Hutuba yake kwa Wananchi wa Bweleo  jimbo la Dimani Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi  wakati alipofanya ziara ya kukabidhi vifaa mbali mbali ya Kilimo cha zao la Mwani,kwa kikundi cha “Ukweli ni Njia  Safi Bweleo” (kulia)Mwenyekiti wa kikundi cha “Ukweli ni Njia  Safi Bweleo” Bi. Safia Hashim Makame na Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “B”Mhe Hamida Mussa Khamis .[Picha na Ikulu] 07/11/2022. 

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi pia Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation “ZMBF”,(kulia) akimkabidhi Mashine ya kusagia Mwani Mwenyekiti wa kikundi cha “Ukweli ni Njia  Safi Bweleo” Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi  Bi. Safia Hashim Makame  (katikati) wakati akiwa katika ziara ya kugawa vifaa vya Mwani leo,wengine kushoto) Mwakilishi wa Jimbo la Dimani Mhe.Mwanaasha K.Juma, akiwepo na Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “B”Mhe Hamida Mussa Khamis,[Picha na Ikulu] 07/11/2022. 

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi pia Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation “ZMBF”,(kushoto) akiangalia bidhaa mbali mbali za zao la mwani alipotembelea katika duka la  kikundi cha “Ukweli ni Njia Safi Bweleo” (kulia) Mwenyekiti wa kikundi   Bi. Safia Hashim Makame   akiwa katika ziara ya kugawa vifaa vya Mwani leo.[Picha na Ikulu] 07/11/2022.

No comments:

Post a Comment