Tetesi za soka Ulaya 10.11.2022 - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Thursday, 10 November 2022

Tetesi za soka Ulaya 10.11.2022

 


Victor

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Mshambulizi wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 23, yuko kwenye rada za Manchester United wanaotafua mshambuliaji kwa ajili ya msimu ujao. (Manchester Everning) Hata hivyo, kikosi hicho cha Old Trafford kinakabiliwa na ushindani kutoka kwa Real Madrid huku meneja Carlo Ancelotti akijaribu kumshawishi rais wa mabingwa hao wa Hispania Florentino Perez kumsajili Osimhen, pamoja na mshambuliaji wa AC Milan na Ureno Rafael Leao, 23, katika dirisha la mwezi Januari. (Sport via Mail)

Manchester United pia wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Argentina Enzo Fernandez, 21, kutoka Benfica. (Record)

Enzo

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Enzo

Liverpool wanavutiwa na mshambuliaji wa Borussia Dortmund Mjerumani Youssoufa Moukoko, 17, ambaye amefunga mabao sita katika mechi 13 msimu huu. (Bild).

Wamiliki wa Newcastle United wako tayari kutumia £70m nyingine kwa ajili ya usajili msimu huu wa joto ili kuendelea kuimarisha kikosi chao. (Sun)

Bayern Munich hawajashawishika kuhusu uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa England na Tottenham Harry Kane licha ya ripoti za mwezi uliopita kudokeza kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 ndiye anayepewa kipaumbele na klabu hiyo ya Ujerumani. (Bild, via The Sun)

Harry Kane

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Harry Kane

Newcastle wanajiandaa kuwasilisha ofa kwa kiungo wa kati wa Velez Sarsfield raia wa Argentina mwenye umri wa miaka 19 Maximo Perrone 'siku chache zijazo'. (Express)

Kiungo wa kati wa Uruguay Facundo Pellistri, 20, anataka kuondoka Manchester United moja kwa moja baada ya kukamilisha kipindi cha mkopo katika klabu ya Alaves ya Uhispania. (Mail)

Antonio Conte anatarajia kusalia Tottenham na atasaini mkataba mpya, anadai msaidizi wake Cristian Stellini. (Evening Standard)

Kiungo Mfaransa wa Borussia Monchengladbach Kouadio 'Manu' Kone anasakwa na West Ham katika dirisha la mwezi Januari. (Bild)

Mykhaylo Mudryk

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Mykhaylo Mudryk

Arsenal watakuwa tayari kutoa kitita kinachotakiwa na Shakhtar Donetsk cha £56m kwa winga wa Ukraine Mykhaylo Mudryk huku The Gunners wakionekana kuwa mstari wa mbele kwenye mbio za kumnasa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (Give me Sport)

Mkufunzi mpya wa Wolves Julen Lopetegui ana nia ya kuwasajili beki wa Uhispania Nacho Fernandez, 32, na mshambuliaji raia wa Dominica Mariano Diaz, 29, kutoka Real Madrid. (Goal)

Chelsea wana nia ya kumsajili beki wa Atletico Madrid raia wa Uruguay Jose Maria Gimenez, 27. (SportWitness)

Newcastle wanavutiwa na mshambuliaji wa Real Betis Mfaransa Nabil Fekir, 29, na ada inasemekana kuwa karibu €50m. (Mundo Deportivo)

No comments:

Post a Comment