Tetesi za soka ulaya 22.11.2022 - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Monday, 21 November 2022

Tetesi za soka ulaya 22.11.2022

 


Gossip

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Liverpool wanamfuatilia Declan Rice wa England kwenye Kombe la Dunia kabla ya kuweka dau la kumnunua kiungo huyo mwenye miaka 23 anayechezea West Ham. (Football Insider)

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola anakaribia kukubali mkataba mpya utakaomuweka klabuni hapo hadi msimu wa joto wa 2025. (Sport - in Spanish)

Mchezaji wa kimataifa wa Uingereza wa Everton Jordan Pickford, 28, na wachezaji wawili wa Hispania David Raya wa Brentford na Robert Sanchez mwenye umri wa miaka 25 wa Brighton wanasakwa na Tottenham ambao pia wanaafuta mbadala wa muda mrefu wa kipa wao mfaransa Hugo Lloris, 35. (90Min).

Gossip

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Chelsea wanakaribia kukamilisha dili la kumnunua Christopher Nkunku, mshambuliaji wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 25 akitikea RB Leipzig tarehe 1 Julai. (Le10 Sport)

Real Madrid hawana mpango wa kumsajili tena mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, 37, kutoka Manchester United kwenye dirisha la mwezi Januari. (Marca)

Newcastle United inamuwania mshambuliaji wa Juventus na Serbia Dusan Vlahovic, 22, ikiwa watafuzu kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao. (Calciomercatoweb)

Gossip

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Bournemouth wanatazamiwa kumteua kocha wa muda Gary O'Neil kama meneja wa kudumu baada ya mazungumzo na mkufunzi wa zamani wa Leeds United Marcelo Bielsa kuvunjika. (Football Insider)

O'Neil anataka kumfanya kocha wa zamani wa Blackpool Neil Critchley kuwa msaidizi wake iwapo atapata kibarua cha kudumu Bournemouth. (Sun)

Mkataba wa kiungo wa kati wa Hispania Marco Asensio na Real Madrid unamalizika msimu wa joto na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 anasema anatumai kuwa anaweza kukubaliana mkataba mpya na klabu hiyo ya Bernabeu, huku uamuzi kuhusu mustakabali wake ukitarajiwa kufanywa baada ya Kombe la Dunia. (Radio Marca, via Goal)

Kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane amekubali kurithi mikoba ya Didier Deschamps kama meneja mpya wa timu ya taifa ya Ufaransa baada ya Kombe la Dunia. (Mundo Deportivo)

Gossip

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Aliyekuwa meneja wa Burnley Sean Dyche ana nia ya kuzungumza na Rangers kuhusu kuifundisha baada ya kumfukuza kocha wao Giovanni van Bronckhorst. (Football Insider)

Paris St-Germain imetuma maskauti kumtazama mshambuliaji wa Arsenal Gabriel Martinelli, 21, akiichezea Brazil kwenye Kombe la Dunia. (Todofichajes)

Tottenham wanafikiria kumnunua kiungo wa kati wa Atalanta mwenye umri wa miaka 29 raia wa Ukraine Ruslan Malinovskyi. (Calciomercato)

Bayern Munich wameulizwa na vilabu kadhaa, ikiwemo Arsenal, kuhusu hali ya winga wa Ujerumani Leroy Sane lakini mabingwa hao wa Bundesliga hawataki kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26. (90Min)

No comments:

Post a Comment