TUME YA MAADILI YATOA MAFUNZO KWA MASHEHA - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Monday, 7 November 2022

TUME YA MAADILI YATOA MAFUNZO KWA MASHEHA

 

Afisa habari kutoka tume ya maadili  ya viongozi Serikalini Halima Jumbe Said akiwasilisha mada ya maadili kwa masheha na madiwani ( hawapo pichani) wa Wilaya ya Mjini  wakati akitoa mafunzo ya maadili katika ukumbi wa skuli ya sekondari Lumumba. Masheha na madiwani kutoka wilaya ya Mjini wakiwasikiliza kwa umakini wakufunzi kutoka tume ya Utumishi Serikalini wakati wakipatiwa mafunzo ya maadili katika ukumbi wa skuli ya sekondari Lumumba. 

Afisa usajili kutoka tume ya maadili  ya viongozi Abdulatif Ali akiwasilisha mada kuhusu mgongano wa kimasilahi kwa masheha na madiwani wa Wilaya ya Mjini wakati akitoa mafunzo katika ukumbi wa skuli ya sekondari Lumumba. Baadhi ya masheha wakiuliza maswali kwa maafisa kutoka tume ya maadili  ya viongozi huko katika ukumbi wa skuli ya sekondari Lumumba.

 **********************

Na Bahati Habibu                    Maelezo  7/11/2022

Viongozi na watumishi wa Umma wametakiwa kufuata misingi na maadili ya Umma ili kuleta maendeleo na kuimarisha utawala bora nchini. 

Akitoa  mafunzo ya Maadili ya Uongozi kwa masheha na madiwani wa Wilaya ya Mjini Unguja huko katika ukumbi wa  skuli ya Lumumba, Afisa Usajili kutoka  Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma  Zanzibar Abdulatif Ali amesema  kufuata misingi na maadili ya umma yana yanapelekea kuwepo uwajibikaji mzuri na uadilifu katika utekelezaji wa majukumu katika jamii

Amesema  maadilii kwa viongozi na watumishi wa umma hujenga uaminifu na utendaji kazi kiufanisi  kwa kuimarisha utawala bora na kuleta maendeleo kwa kukuza wa nchi

Afisa huyo ameleza lengo la mafunzo hayo ni kuwaweka viongozi na watumishi wa umma kufuata misingi na maadili umma  na kutokuvunja sheria  ya maadili ya umma ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji.

“Mgongano wa maslahi ni miongoni mwa matatizo yanayorejesha nyuma maendeleo ya nchi na kuhakikisha wanafanya majukumu yao bila ya upendeleo kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa na tume hiyo”, amefahamisha Afisa huyo.

Nae Afisa Habari wa Tume Halima Jumbe Said amewasisitiza viongozi hao kuyatumia mafunzo ya maadili ya umma ili kuwa viongozi bora na kuleta maendeleo  ya nchi.

Amewataka viongozi hao kuzitumia vyema nyadhifa zao walizopewa katika kuwatunikia wananchi na kuacha tabia ya kujipatia maslahi binafsi kwa lengo la kuleta maendeleo katika jamii.

Nao masheha hao  wameiomba tume ya Maadili kuwapatia viongozi wa umma mwongozo wa  Sheria utakaowasaidia katika kutekeleza majukumu  kwa uweledi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here