KIGAHE AWATAKA WAWEKEZAJI SEKTA YA VIWANDA KUTUMIA TEKNOLOJIA RAFIKI KUPUNGUZA HEWA YA UKAA. - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Tuesday, 6 December 2022

KIGAHE AWATAKA WAWEKEZAJI SEKTA YA VIWANDA KUTUMIA TEKNOLOJIA RAFIKI KUPUNGUZA HEWA YA UKAA.

 Naibu Waziri wa Uwekezaji ,Viwanda na  Biashara,Exaud Kigahe akizungumza katika mkutano  huo jijini Arusha .

************************
Arusha.Naibu Waziri wa Uwekezaji ,Viwanda na  Biashara,Exaud Kigahe amewataka wawekezaji wanaoshindana  katika sekta ya viwanda,ndege na makampuni ya  utalii kutumia teknolojia rafiki ili kupunguza utoaji wa hewa ya ukaa inayochangia mabadiliko hasi ya tabia nchi.
Hayo yamesemwa  leo jijini Arusha na Naibu Waziri Kihage wakati wa ufunguzi wa kongamano la madhimisho ya Ushindani Duniani katika kilele cha siku ya ushindani Duniani.
Amesema endapo endapo kampuni hizo zitazingatia matumizi sahihi ya matumizi ya hewa ukaa itasaidia kupunguza hewa ukaa inayochangia mabadiliko ya tabia nchi.
Amesema  lengo la wafanyabiashara wote ni kupata faida hivyo lazima kuhakikisha ushindani wa haki unazingatiwa ikiwemo kuhakikisha mamlaka ya ushindani zinazuia ukiritimba katika biashara ikiwemo nguvu ya soko kuwameza washindani katika biashara.
Pia kudhibiti muingiliano wa biashara katika unaolenga kuwaweza washindani katika baadhi ya biashara na kuongeza kuwa ongezeko la mabadiliko ya tabia nchi unahatarisha usalama na uhatarishi wa theluji katika mlima Kilimanjaro.
“Wawekezaji katika sekta ya Viwanda,ndege na makampuni ya utalii kutumia teknolojia rafiki katika kudhibiti mazingira ikiwemo wanyama katika sekta ya utalii katika upunguzaji wa ikolojia ya wanyama ikiwemo ukataji ovyo wa miti ikiwemo mkaa “amesema Kigahe.
Ametoa rai kwa wadau mbalimbali kupanda miti ili kudhibiti uongezeko la hewa ukaa hivyo ni lazima miti ipandwe katika kulinda ikolojia ya wanyama sanjari na uoto asili
Naye Mwenyekiti wa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC),Dk,Aggrey Mlimuka amesema kuwa, kongamano hilo ni muhimu katika kuhakikisha kunakuwa na uendelevu na ushindani katika kuhakikisha utalii unakua kwa kasi sanjari na ulinzi wa mazingira
“kauli mbiu ya mwaka huu ni ushindani na maendeleo endelevu kwani kuwepo kwa Utalii huo endelevu kuna hitaji juhudi za pamoja katika kulinda mazingira ikiwemo ufanyaji biashara na kuleta ushindani.”amesema 
Naye  Jaji Salma Maghimbi kutoka Baraza la Ushindani ametoa rai kwa mawakili kuhakikisha wanazingatia kanuni na sheria katika uendeshaji wa kesi za ushindani katika kuhakikisha kesi zinasikilizwa na kutolewa maamuzi.
Awali Kaimu Mkuu wa wilaya ya Arusha,Injinia Richard Ruyango ametoa rai kwa wadau mbalimbali katika sekta ya mazingira kuhakikisha mazingira yanalindwa ili kuzuia chagamoto za mabadiliko ya tabia nchi na ikolojia.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here