Chelsea wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Atletico Madrid Joao Felix ambapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 anaweza kuwasili kwa mkopo mwezi Januari kukiwa na kipengele cha kumnunua moja kwa moja mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno katika msimu wa joto. (Telegraph)
Liverpool imefikia makubaliano ya kumsajilli mshambuliaji mholanzi Cody Gakpo kutoka PSV Eindhoven. Gakpo, 23, anatua kwa dau la kati ya £35.4m-£44.3m (Fabrizio).
Klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia imepanga kumfanyia vipimo vya afya mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, 37, kabla ya kukamilisha uhamisho wake wa $75m kwa mwaka. (CBS Sports).
Arsenal wamewasilisha dau la pauni milioni 55 kwa ajili ya kumnunua winga wa Shakhtar Donetsk na Ukraine Mykhaylo Mudryk, 21. (Telegraph).
Mykhaylo Mudryk
Kocha wa West Ham David Moyes anasema klabu hiyo "haitayumba tu" na kumwachia kirahisi kiungo wa kati wa England Declan Rice, 23, kuondoka msimu wa joto. (Mail)
Ajax wamewasiliana na kipa wa Brentford na Hispania David Raya, 27, kuhusu uwezekano wa kumsajili katika dirisha la Januari. (AS)
Barcelona hawako tayari kumuuza kiungo wa kati wa Uholanzi Frenkie de Jong, 25, ambaye alikuwa akisakwa na Manchester United katika dirisha lililopita la msimu wa joto. (Sport)
Everton ni miongoni mwa vilabu kadhaa vya Ligi kuu England vinavyoonyesha nia ya kumnunua winga wa Manchester United na Uswiswi Anthony Elanga, 20. (Mail)
Anthony Elanga
Mshambulizi wa Ureno Rafael Leao, 23, anasema angependa kucheza katika Ligi ya England katika siku zijazo lakini "sasa niko AC Milan kwa 100%. (RDP Africa, via Talksport)
Brentford, Fulham na Aston Villa wametoa ofa kwa shambuliaji wa Chicago Fire na Colombia Jhon Duran, lakini Benfica wako katika nafasi nzuri ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19. (Calciomercato)
Chelsea wapo kwenye mazungumzo ya mwisho ya kumsajili beki wa kati wa Monaco na Ufaransa Benoit Badiashile na wamewasilisha ofa rasmi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (Fabrizio Romano)



No comments:
Post a Comment