Katibu mkuu wa chama cha mapinduzi CCM Daniel Chongolo amemtaka mkandarasi anayejenga mradi wa barabara ya kutoka ruaha kilombero na daraja kubwa la ruaha mkuu, kuhakikisha anakamilisha Ujenzi huo Kabla ya Oktoba mwaka huu, ili hatimae Wananchi katika Wilaya za Kilosa, Kilombero, Ulanga pamoja na Malinyi wanufaike kupitia shughuli mbalimbali za kiuchumi kwenye maeneo yao.
Chongolo ametoa kauli hiyo leo wakati akikagua Mradi huo wa Ujenzi wa Barabara na Daraja wenye urefu wa Kilomita 66.9, ambao umegharimu kiasi cha Fedha Shilingi Bilioni 105, ambapo amesema dhamira ya Serikali ya CCM ni kuwaletea maendeleo Watanzania kwa kuwaondolea Changamoto ikiwemo za Miundombinu mbali mbali.
Katika hatua nyingine Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amemuagiza mkuu wa mkoa wa Morogoro Fatuma Mwasa kuangalia utaratibu mzuri wa wakulima wa miwa kutoka kila AMCOS kujifunza namna ya Kutambua kiwango cha Utamu wa Miwa ili kuondoa Malalamiko kwa Wakulima hao wanaouza Miwa yao katika kiwanda cha Sukari Kilombero.
Hiyo ni Baada ya Kuibuka kwa Malalamiko ya Wakulima Wilayani Kilombero kukosa imani na zoezi la Upimaji wa kiwango cha Utamu, kwa madai hupewa malipo kidogo.
Chongolo yupo katika ziara ya kikazi mkoani Morogoro akiwa ameongozana na na Katibu wa Halmashauri Kuuya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema na Katibu wa NEC Oganaizesheni, Issa Haji(Gavu).
No comments:
Post a Comment