Chen Chien-jen atakuwa Waziri Mkuu mpya wa Taiwan - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Wednesday, 25 January 2023

Chen Chien-jen atakuwa Waziri Mkuu mpya wa Taiwan

 


Chen Chien-jen ambaye anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu mpya wa Taiwan

Hatua hii imekuja kufuatia Waziri Mkuu Su Tseng-chang aliyewasilisha barua yake ya kujiuzulu wiki iliyopita pamoja na ile ya baraza lake la mawaziri kabla ya kuundwa upya kwa serikali inayotarajiwa kuwa na mabadiliko

Makamu wa Rais wa zamani Chen Chien-jen atakuwa Waziri Mkuu mpya wa Taiwan, ofisi ya rais imesema Jumatano kama sehemu ya mabadiliko ya baraza la mawaziri kufuatia kushindwa vibaya kwa chama tawala cha Democratic Progressive Party (DPP) katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka jana.

Waziri Mkuu Su Tseng-chang aliwasilisha barua yake ya kujiuzulu wiki iliyopita pamoja na ile ya baraza lake la mawaziri kabla ya kuundwa upya kwa serikali inayotarajiwa kuwa na mabadiliko.

Hatua hiyo ya Su ilifuatia hatua ya DPP kutofanya vizuri katika uchaguzi wa ndani mwezi Novemba, na inakuja wakati Taiwan ikijiandaa kwa uchaguzi wa rais na bunge mapema mwaka 2024.

Rais Tsai Ing-wen anatarajiwa kufanya mkutano na waandishi wa habari Ijumaa asubuhi kutoa tangazo rasmi, ofisi yake imesema katika taarifa fupi, lakini bila kutoa maelezo ni nafasi zipi nyingine zitapata mawaziri wapya.

Chen mwenye umri wa miaka 71 ni muumini wa kikatoliki ambaye alihudumu kama Makamu wa Rais wakati wa muhula wa kwanza wa Tsai madarakani kuanzia 2016 hadi 2020 na vyombo vya habari vya Taiwan vilimtaja kama mtu anayeweza kuwa Waziri Mkuu mpya.

Atalazimika kusimamia masuala kadhaa yenye utata ikiwa ni pamoja na uchumi wa kisiwa unaoyumba na mipango ya kupanua usajili wa kijeshi hadi mwaka mmoja kutokana na kuongezeka kwa tishio la kijeshi kutoka China ingawa DPP ina idadi kubwa ya viti bungeni ikimaanisha mapendekezo yake yatapitishwa bila kusita.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here