Dhoruba kubwa yasababisha vifo vya watu 16 California - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Wednesday, 11 January 2023

Dhoruba kubwa yasababisha vifo vya watu 16 California

 


Wafanyakazi wa kituo cha umeme cha Wilaya ya Sacramento, California wanatengeneza waya za umeme zilizoanguka kufuatia dhoruba, Januari 9, 2023. Picha ya Reuter

Dhoruba zisizosita zimelikumba tena jimbo la California Jumanne, ikiwa hali mbaya zaidi ya hewa ya hivi karibuni ambayo imesababisha vifo vya takriban watu 16 na kusababisha uharibifu katika eneo kubwa.

Mvua kubwa iliyonyesha ilisababisha mafuriko, kufungwa kwa barabara kuu, na kuangusha miti na kusomba madereva na abiria, akiwemo mvulana wa miaka mitano ambaye bado hajulikani aliko katikati mwa California, huku mvua na theluji zaidi ikitarajiwa kulikumba jimbo hilo lenye wakazi wengi zaidi hapa Marekani.

Karibu nyumba 160,000 na biashara hazikuwa na umeme Jumanne, kulingana na tovuti inayofuatilia kukatika kwa umeme, Poweroutage.us.

Dhoruba nyingine yenye ukubwa wa inchi saba za mvua inatazamiwa kulikumba jimbo hilo kaskazini mwa California leo Jumatano, na kutakuwa na theluji kubwa zaidi katika milima ya Sierra Nevada, idara ya kitaifa ya hali ya hewa imesema.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here