Kwanini Arsenal wanaudhibiti uongozi wa ligi ya Premia - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Monday, 16 January 2023

Kwanini Arsenal wanaudhibiti uongozi wa ligi ya Premia

 


.

CHANZO CHA PICHA,BBC SPORT

Maelezo ya picha,

Jedwali la ligi

Arsenal wanapigiwa upatu kushinda Ligi Kuu sasa. Ni wazi ssa kwamba watasalia katika kilele cha jedwali la liugi ya England kwa muda.

 

Kitu pekee ambacho hatujui kuhusu kikosi cha Mikel Arteta ni jinsi watakavyokabiliana na kuwa viongozi wa ligi katika kipindi cha pili cha msimu.

 

Lakini haionekani kuwa ukosefu wao wa uzoefu wa kuwa katika mbio za kuwania ubingwa wa ligi unawashangaza kwa sasa .

 

Ushindi wao mzuri zaidi dhidi ya wapinzani wao wa London kaskazini Tottenham siku ya Jumapili ulikuwa uthibitisho zaidi ya hilo.

 

Katika kipindi cha kwanza tuliona nia yao ya kushambulia na ubunifu, wakiwabana Spurs kuwaweka kwenye nusu yao uwanja na kisha kutumia makosa yao.

 

Arsenal walikuwa na kibarua kigumu cha kuimarisha safu yao ya ulinzi katika kipindi cha pili lakini walikuwa wazuri bila mpira na, Tottenham walijaribu kushambulia , Aaron Ramsdale alikuwa mlinda lango mzuri aliyewazuia.

 

Nilifurahishwa sana na timu yao yote, kutoka mbele hadi nyuma, na inaonekana kwamba  wana uwezo unaohitajika – pa,poja na ari ya ya kutaka kufunga – ambacho watahitajika katika kipindi cha miezi michache iliopita.

.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Nahodha wa Arsenal Martin Ordegard

Kuwa mbele kwa pointi nane baada ya mechi 18 ni mafanikio ya makubwa kwa timu hii ya Arsenal - na inastahili kwa kwli.

 

Sasa wanapaswa kujaribu kusalia huko, na wachezaji wao wengi tayari wamejifunza kwa bidii jinsi mambo yanaweza kubadilika haraka. Walianguka katika wiki za mwisho za msimu uliopita, walikosa kumaliza katika nafasi nne za juu na kurejea Ligi ya Mabingwa walipokuwa ndani ya uwezo huo.

 

Lakini tangu kuanza kwa kampeni hii nimekuwa nikisema hii inaonekana kama timu tofauti ya Gunners kulingana na mawazo yao, na Arteta na timu yake ya kufundisha wana uzoefu wa mwaka mwingine pia.

 

Arteta amekusanya kikosi chenye vipaji, chenye mtazamo bora na wanaonekana kustareheshwa sana na kile anachotaka wafanye.

 

Pamoja na nia yao kubwa ya kutaka kushinda, wapo imara katika kila nafasi na wameweza kukabiliana na kila jeraha walilopata, akiwemo Gabriel Jesus ambaye alikuwa muhimu kwao mwanzoni mwa msimu, lakini hajacheza tangu Kombe la Dunia. . Eddie Nketiah ameongozasafu ya mbele  vizuri sana, ina maana hawajamkosa Jesus.

 

Kwa busara, inaonekana kama Arteta yuko tayari kwa chochote pia. Bila shaka alimfikiria zaidi kocha wa Spurs Antonio Conte na mpango wake wa mechi Jumapili, haswa katika kipindi cha kwanza wakati ilionekana kama Arsenal walikuwa na mtu wa ziada katika kila eneo la uwanja.

.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Kikosi cha kwanza cha Arsenal

Bila shaka bado kuna vikwazo vikubwa vya kuvuka: bado wanapaswa kucheza na Manchester City mara mbili na, kabla ya hapo, watakabiliana na Manchester United inayofufuka wikendi ijayo.

 

Lakini kila mchezo ni mkubwa unapokuwa juu na kwa sasa wanaonekana kuwa na nguvu sana dhidi ya yeyote wanayecheza naye. Wamejaa ujasiri na hivi sasa ni vigumu kuwazuia.

Je Man United inaweza kuwa mgombea wa taji la ligi?

Wikiendi nzima ilikwenda vizuri sana kwa Arsenal - inasaidia kila wakati mambo yanapoenda kombo kwa wapinzani wako wa karibu wa taji, kama ilivyokuwa kwa City na kushindwa kwao katika mechi ya Jumamosi ya Manchester.

 

Mabingwa hao watetezi hawakubahatika baada ya bao la United la kusawazisha, ambalo nilihisi lilipaswa kuwa la kuotea , na bao hilo lilibadilisha mchezo kabisa.

 

Bado sioni City wawachilia  ubingwa wao bila pambano, na sio wao pekee ambao wanaweza kuwapa changamoto Arsenal kutoka hapa.

 

Ninaelewa kwa nini watu wanaizungumzia Manchester United tena, kwa sababu wamepata mbawa  kwa sasa, kwa kasi kubwa ya matokeo, na Erik ten Hag amefanya maendeleo ya ajabu na timu yake kwa muda mfupi.

 

Kwa sasa huwezi kuwaondoa United, kwa sababu wataenda Emirates Stadium Jumapili ijayo. Watakapoibuka washindi itabidi useme wako sawa katika kuwinda, lakini, kwa upande mwingine, ikiwa Arsenal itawashinda basi matumaini yao ya ubingwa yatakwisha.

 

Kama Manchester United, Newcastle United wako nyuma kwa pointi moja tu, lakini wamecheza mechi moja zaidi.

 

Singehesabu Newcastle kama wagombeaji wa taji, ingawa. Kwa kweli bado nadhani itakuwa miujiza iwapo watamaliza katika nafasi nne za juu, licha ya matatizo yanayokumba baadhi ya timu zilizo chini yao.

 

Kichapo cha Tottenham siku ya Jumapili kilikuwa habari njema kwa kikosi cha Eddie Howe, kwa sababu Spurs wamo katika kundi hilo la kufukuzia na wanasalia kuwa tishio. Tuliona walivyomaliza msimu uliopita kwa kuinyima Arsenal nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa.

 

Pia ninashuku kuwa Chelsea itaimarika baada ya kipindi kibaya katika wiki chache zilizopita, wachezaji wao wanaporejea kutoka kwenye majeraha, lakini Liverpool wanaonekana kutofanya hivyo kwa sasa.

 

Kwa sasa kikosi cha Jurgen Klopp ni kibaya sana nyuma, hakina ukali wanaposhambulia.

 

Wanaonekana kama kivuli cha upande ambao tumezoea kuuona kwenye sehemu ya juu ya jedwali, na sioni mambo yakiboreka hivi karibuni - utakuwa msimu mrefu na mgumu kwao.

Napendelea Newcastle kushinda kikombe kuliko kumaliza katika nafasi nne za juu

Mashabiki wa Newcastle wana wakati tofauti sana wa mambo yalivyo  hivi sasa, bila shaka, na ninafurahia kila dakika yao.

 

Howe anafanya kazi nzuri na alipata matokeo mengine makubwa wikendi hii, na ushindi wao wa dakika za mwisho dhidi ya Fulham.

 

Tangu mwanzo, ilikuwa shangwe kutoka kwa wachezaji na hata kwa mashabiki - ambapo ilieleweka kufuatia msisimko wa ushindi wa katikati ya wiki dhidi ya Leicester ambao uliiweka Newcastle katika nusu fainali ya Kombe la Carabao.

 

Newcastle hawakucheza vyema Jumapili na walihitaji bahati kidogo kwa mkwaju wa penalti uliopigwa vibaya na  Aleksandar Mitrovic, lakini ilikuwa tu kupata pointi tatu na haijalishi jinsi walivyozipata.

 

Kumaliza katika nafasi za Ligi ya Mabingwa itakuwa vyema sana lakini ni nafasi ya kupata kikombe ndio yenye  maana zaidi kwangu.

 

Ndoto yangu kwa msimu huu itakuwa kombe - ningependelea zaidi Kombe la Carabao kuliko nne bora.

 

Ningependa kuona zote mbili zikifanyika, ni wazi, lakini nipe chaguo na ningetafuta kikombe  fedha siku nzima. Ni muhimu zaidi kwangu.

 

Taji la mwisho Newcastle kushinda lilikuwa Kombe la Fairs - mashindano ambayo hatimaye yaligeuka kuwa Ligi ya Europa - mnamo 1969.

 

Hiyo ilikuwa kabla sijazaliwa, kwa hiyo imekuwa ni kusubiri kwa muda mrefu sana kuona tunashinda kitu. Natumai tutafanikiwa  hivi karibuni.

 


No comments:

Post a Comment