Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema kwamba nchi yake itatuma vifaru vya kijeshi vyenye nguvu vinavyojulikana kama Leopard 2 kwa wanajeshi wa Ukraine.
Scholz ameliambia baraza la mawaziri kwamba Ujerumani itatuma vifaru 14, pamoja na kutoa ruhusa kwa nchi nyingine kutuma vifaru hivyo Ukraine.
Hatua ya ujerumani inajiri kutokana na shinkizo za kimataifa kutoka Kyiv na washirika wake kutaka vifaru vilivyotengenezwa Ujerumani wapewe wanajeshi wa Ukraine wanaopigana na wanajeshi wa Russia.
Utawala wa rais wa Marekani Joe Biden unatarajiwa kutangaza hatua ya Marekani kutuma magari zaidi ya kivita kwa wanajeshi wa Ukraine.
Rais Volodymyr Zelensky anaamini kwamba Ukraine inahitaji vifaru 300 ili kuweka kuwashinda nguvu wanajeshi wa Russia.
Balozi wa Russia nchini Marekani amesema kwamba Ukrtaine itauchukulia msaada wa vifaru kwa Russia kuwa uchokozi wa moja kwa moja.
Lavrov amewasili Angola katika ziara Afrika
Wakati huo huo waziri wa mambo ya nje wa Russia Sergei Lavrov amewasili Angola leo jumanne kwa mazungumzo ya kidiplomasia kati ya Angola na Russia.
Vyombo vya habari vya Angola vimeripoti kwamba kuna wasiwasi kwamba Moscow ina hasira kutokana na hatua ya hivi karibuni ya serikali ya Angola kuashiria kutaka kupinga uvamizi wa Russia nchini Ukraine.
Angola haijatangaza msimamo wake kuhusu vita vya Ukraine lakini mnamio mwezi Septemba mwaka uliopiya, ilikosoa hatua ya Russia kujitengea sehemu za Ukraine na kutaka Moscow kukomesha vita hivyo.
Larov anatarajiwa kukutana na rais wa Angola Joao Lourenco katika ikulu yar ais mjini Luanda.
Viongozi hao wawili wanatarajiwa kujadiliana kuhusu uhusiano kati ya nchi hizo mbili
No comments:
Post a Comment