Washukiwa wanajihadi wamewateka takriban wamawake 50 katika eneo lililoharibiwa na uasi kaskazini mwa Burkina Faso, maafisa na wakazi waliiambi AFP jana Jumapili.
Takriban 40 walikamatwa karibu na eneo la kusini mashariki mwa Arbinda, Alhamisi, na wengine 20 walitekwa Ijumaa kaskazini mwa mji kwa mujibu wa chanzo ambacho hakikutaka kutajwa.
Baadhi yao walifanikiwa kutoroka na kurejea katika vijiji vyao na kutoa taarifa walisema.
Taifa hilo lisilo na ufukwe la Afrika magharibi ni moja ya mataifa masikini sana na lililokumbwa na ghasia duniani.
Toka mwaka 2015, limekuwa likijitahidi kupambana na wanamgambo wenye msimamo mkali wenye uhusiano na Alcaida, na kundi la Islamic State ambalo limeua maelfu ya watu na kusababisha wengine takriban milioni mbili kukimbia makazi yao. mmkk
No comments:
Post a Comment