Gumzo la Urithi wa madaraka lazuka Korea Kaskazini baada ya binti wa Kim Jong-Un kuonekana - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Thursday, 9 February 2023

Gumzo la Urithi wa madaraka lazuka Korea Kaskazini baada ya binti wa Kim Jong-Un kuonekana

 


Kim Jong Un na binti yake

CHANZO CHA PICHA,KCNA

Siku ya Jumatano usiku misururu ya makombora makubwa ilipita katika mji mkuu wa Korea Kaskazini Pyongyang. Lakini sio silaha zake pekee ambazo Kim Jong-Un alikuwa akiangazia. Kwenye onesho pia, alikuwa binti yake.

Kiongozi wa Korea Kaskazini alipochukua nafasi yake ya kawaida ya gwaride, katikati ya roshani, aliungana katika hali isiyokuwa ya kawaida na msichana aliyevalia nguo nyeusi.

Anafikiriwa kuwa mtoto wake wa pili, anayeitwa Kim Ju-ae, mwenye umri wa karibu miaka 10.

Hii ni mara ya tano kwake kuonekana hadharani, na yote haya yanafanyika katika muda wa chini ya miezi mitatu.

Katika kipindi hiki kifupi amepitia mabadiliko ya ajabu, na kufanya uwezekano mkubwa kuwa amechaguliwa kuwa kiongozi wa baadaye wa Korea Kaskazini.

Alipotokea kwa mara ya kwanza, mnamo Novemba mwaka jana, wakati wa uzinduzi wa kombora la balestiki linalozunguka mabara (ICBM), uvumi ulikuwa mwingi. Wengi walinong’onezan: Je, msichana huyu siku moja ataongoza taifa hili lenye usiri zaidi duniani?

Lakini wakati huo ilikuwa vigumu kufikiria hivyo kwasababu alionekana mdogo sana. Labda Bw Kim alitaka tu kujionyesha kama baba mzuri au kuonyesha hadharani familia yake, pamoja na silaha zake zote.

Lakini kwa kila anapojitokeza hadharani binti huyo wa Kim anaonekana kukua kimo.

Kim Jong Un na binti yao

CHANZO CHA PICHA,KCNA

Jumanne usiku, kabla ya gwaride, alihudhuria karamu ya maafisa wakuu wa kijeshi wa Korea Kaskazini.

Safari hii alivalia shati jeupe na suti nyeusi yenye vifungo, huku nywele zake zikiwa zimechanwa kwa nyuma.

Picha hizo ziliwavutia watu wengi wa Korea Kaskazini. Katika kila picha anapanda jukwaa la kati, akiwa ameketi kati ya mama yake na baba yake, na kuzungukwa na maafisa wa kijeshi.

Jambo lingine la kustaajabisha limekuwa lugha inayotumiwa kumuelezea Bi Kim.

Alitambulishwa kwa mara ya kwanza kwenye vyombo vya habari vya serikali kama binti "mpendwa" wa Kim Jong-Un.

Kufikia karamu ya kijeshi ya Jumanne alikuwa amepandishwa hadhi ya binti wa "kuheshimiwa". Ni kivumishi kilichotengwa kwa ajili ya wale tu wanaoheshimika zaidi.

Ni baada tu ya hadhi ya Kim Jong-Un kama kiongozi wa baadaye kuimarishwa, ndipo alipoitwa "rafiki anayeheshimiwa".

Tangu kuanzishwa kwake, Korea Kaskazini imetawaliwa na vizazi vitatu vya familia ya Kim. Raia wake wanaambiwa kuwa familia hiyo inatoka katika ukoo wa damu takatifu, ikimaanisha ni wao pekee wanaoweza kuongoza nchi. Kim Jong-Un atataka kuhakikisha anapitisha uongozi hadi kizazi cha nne.

Lakini hata kama Bi Ju-ae ndiye mrithi aliyekusudiwa, kwa nini umtambulishe mapema sana, na kwa kasi hiyo? Kim Jong-Un ana umri wa miaka 39 pekee - binti yake bado mtoto.

Inasemekana kwamba Bw Kim alifichuliwa kama mrithi wa babake Kim Jong-Il alipokuwa na umri wa miaka minane, lakini kwa faragha tu kwa viongozi wa kijeshi.

Hadharani, iliwekwa wazi takriban mwaka mmoja kabla ya baba yake kufariki. Hii ilimpa mwanzo mbaya wa kazi, kwani alifanya kazi kwa ukatili ili kuimarisha utawala wake.

Labda anajaribu kumrahisishia kazi binti yake, kwa kuhakikisha msimamo wake umeimarishwa zaidi wakati anachukua hatamu ya uongozi. Labda afya yake haiko katika hali nzuri, na hana muda mrefu kama tunavyofikiria.

Gumzo liliibuka wakati Kim Ju-ae alipopewa nafasi  ya kukaa kati ya babake Kim Jong-Un na mkewe Ri Sol-Ju wakiwa kwenye karamu ya kijeshi.

CHANZO CHA PICHA,KCNA

Maelezo ya picha,

Gumzo liliibuka wakati Kim Ju-ae alipopewa nafasi ya kukaa kati ya babake Kim Jong-Un na mkewe Ri Sol-Ju wakiwa kwenye karamu ya kijeshi.

Sababu nyingine ambayo Kim Jong-Un anaweza kuhitaji muda mwingi kutekeleza, ni kuondokana na ubaguzi wa kile ambacho ni jamii ya mfumo dume.

Korea Kaskazini haijawahi kuongozwa na mwanamke, licha ya kuwa na baadhi ya wanawake katika nafasi za juu - dadake Kim Kim Yo-Jong ndiye mfano maarufu zaidi.

James Fretwell, mchambuzi wa jukwaa la ufuatiliaji la Korea Kaskazini NK News, hafikirii kuwa hii haiwezi kufanyika.

"Wakati Korea Kaskazini ni jamii inayotawaliwa na wanaume, pia ni jamii inayotawaliwa na Kim," aliambia BBC. "Zaidi ya yote, ukoo wa utamfanya mgombea wake wa uongozi. Itashangaza zaidi ikiwa mtu wa nje ya familia tawala ya Kim-mwanaume au mwanamke- angeweza kuchukua nafasi ya juu."

Hiyo ilisema, kumsimamisha mwanamke juu kabisa kutahitaji kazi ikiwa atakubaliwa kikweli na watu, wanajeshi, na wasomi.

Nafasi ya Kim Ju-Ae kama kiongozi ajaye wa Korea Kaskazini haijahakikishiwa, lakini kila anapoonekana hadharani ishara zote zinaelekea kwa uongozi ujao.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here