SPIKA DKT. TULIA APOKEA TUZO YA UENEZI WA KISWAHILI, AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKAZI WA KAMPUNI YA HUAWEI NCHINI - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Thursday, 9 February 2023

SPIKA DKT. TULIA APOKEA TUZO YA UENEZI WA KISWAHILI, AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKAZI WA KAMPUNI YA HUAWEI NCHINI

 

Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akipokea tuzo ya uenezi wa kiswahili kutoka kwa Naibu Rais wa Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU), Dkt. Mussa Hans kwa niaba ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutambua jitihada za Bunge katika matumizi ya Kiswahili katika mijadala Mbalimbali ya Kibunge. Kuanza kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Ndg. Consolata Mushi, Rais wa Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU), Mhe. Salma Kikwete na Mbunge wa Mlalo ambaye pia ni Katibu wa Wabunge wa CCM, Mhe. Rashid Shangazi katika tukio lililofanyika leo tarehe 9 Februari, 2023 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Kampuni ya Huawei Nchini, Ndg. Tao Mian (kulia kwake) pamoja na Mkurugenzi wa Mahusiano wa Huawei Nchini, ndg. Ma Shengjie walipomtembelea ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma leo tarehe 9 Februari, 2023, Baada ya mazungumzo yaliyofanyika ofisini hapo.

- Advertisement -

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here